Kyela: Wananchi Kilombero waamua kujenga ofisi ya mwalimu mkuu
23 May 2024, 19:08
Wananchi wamesema wameanza kuchangishana fedha ili kuhakikisha wanafanikisha ujenzi wa ofisi ya mwalim mkuu katika shule ya msingi kilombero kata ya Mababu hapa wilayani Kyela.
Baada ya Halmashauri ya Wilaya ya kyela kukusudia kusaidia fedha za kukamilisha ujenzi wa vyumba vitatu vya madarasa katika shule ya msingi kilombero wananchi wameanza kujipanga kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya Mwalimu mkuu.
Akizungumza na Mwandishi wa habari Mwenyekiti wa kijiji hicho Yahaya Twaha amesema,baada ya wananchi kujenga vyumba vya madarasa hadi kufikia hatua ya linta kinachosubiliwa ni mpango wa halmashauri kukamilisha ujenzi huo ifikapo mwezi wa saba,huku wananchi wakijiandaa na ujenzi wa ofisi ya mwalimu Mkuu wa shule hiyo.
sauti ya mwenyekiti wa kijiji yahaya Twaha akielezea mipango mikakati ya ujenzi wa nyumba ya mwalimu mkuu
Twaha ameongeza kuwa,wananchi wamekuwa mstari wa mbele katika kushiriki shughuli za maendeleo katika shule hiyo,ambapo mpaka sasa nguvu za wananchi wamefanikiwa kukusanya mawe pamoja na kuchanga fedha kwa ajili ya ununuzi wa tofali na kuzifikisha eneo la shule,ambapo mahitaji yaliyobakia kukamilisha jengo hilo ni mabati,simenti na vifaa vingine.
sauti ya mwenyekiti Twaha akielezea jinsi mbunge wa jimbo la kyela alivyo toa msaada wake
Mbali na changamoto hizo wananchi wa kijiji hicho wamemshukuru Mbunge wa jimbo la kyela Ally Mlaghila Jumbe kwa kutoa msaada wa mabati mia moja,ambapo wito umetolewa kwa wadau wengine kusaidia vifaa kwa kuwa Mbunge amefungua njia ya wadau wengine.
mwenyekiti twaha akiwaomba wadau msaada wa kukamilisha ujenzi
Shule ya msingi kilombero iliyopo kijiji cha kilombero kata ya mababu wilaya ya kyela ina jumla ya wanafunzi zaidi ya mia tatu huku walimu wa kuajiliwa wakiwa watano na mmoja wa kujitolea.