Kyela: Likambo mlemavu wa viungo anayelea watoto 10 kwa baiskeli, pikipiki
20 May 2024, 18:35
“Nilipata ulemavu nikiwa na umri wa miaka thelathini nikiwa na mke na watoto watatu.” Anaeleza Mwambungu
Na Masoud Maulid
Watanzania wenye ulemavu wametakiwa kujishughulisha na shughuli ndogondogo za ujasiriamali na kuachana na tabia ya ombaomba ili kukidhi mahitaji yao.
Kauli hii inakuja baada ya kuwepo kwa baadhi ya jamii ya watanzania wenye ulemavu wa viungo kuona ulemavu wao ni sababu ya wao kuomba kwa watu badala ya kujishughulisha kufanya kazi zitakazowaingizia kipato.
Mfano mzuri wa kuigwa ikawa ni Adam Mwambungu maarufu Likambo ambaye licha ya kupata ulemavu wa viungo kwa miaka 22 sasa bado ni mjasiriamali ambaye ameweza kumudu na kutunza familia ya watoto kumi wakiwemo na watoto wa ndugu zake.
Undani wa habari hii tunaungana na mwandishi wetu Jamila Mwambande ambaye ametuandalia taarifa fupi kutoka Kisale hapa wilayani Kyela.