KARAGWE FM PROFILE
UTANGULIZI.
Radio Karagwe ni Radio ya kijamii iliyoanzishwa na shirika lisilokuwa la kiserikali lijulikanalo kama Karagwe Media Association (KAMEA).Ilianza kurusha matangazo yake Desemba 11.2007 kupitia masafa ya 91.4 MHz kwa ufadhili wa shirika la nchini Denmark (ULD80 Karagwe Venor) waliowezesha mafunzo kwa watumishi na upatikanaji wa vifaa.
DIRA.
Kuziba pengo la mawasiliano kwa wananchi wa Karagwe ambao kwa wakati huo hawakuwa na uwezo wa kusikiliza radio za Tanzania kutokana na jiongrafia ya eneo.
MAENEO REDIO INAKOSIKIKA
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na ULD80 June mwaka 2012 Radio Karagwe ina zaidi ya wasikilizaji milioni 1.2.(KM 200 KUTOKA MAKAO MAKUU).Inasikika katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Kagera,katika wilaya za Karagwe, Kyerwa, Missenyi, Muleba na Bukoba Vijijini. Inasikika katika maeneo machache wilaya za Ngara, Biharamulo na Bukoba manispaa. Pia inasikika maeneo ya nchi jirani za Uganda, Burundi na Rwanda.
MAWASILIANO.
S.L.P 316,KARAGWE KAGERA TZ
E-mail : radiokaragwe@gmail.com
Phone: +255 754 677 708 / +255 689 471 171