Recent posts
28 April 2021, 2:40 pm
Bilioni 82 zatengwa kwa ajili ya miradi.
Manispaa ya Mji wa Bukoba imetenga jumla ya shilingi bilioni 82 kwaajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali itakayosaidia kukuza uchumi na kuleta maendeleo ya wananchi. Hayo yamebainishwa na Mstahiki Meya wa Manispaa ya Bukoba Godson Rwegasila Gypson ambaye pia ni…
28 April 2021, 1:49 pm
Madereva walia na ubovu wa stendi.
Madereva wa Tax katika stendi ya Kayanga wilaya ya Karagwe Mkoa Kagera wameiomba serikali wilayani humo kufanya marekebisho ya stendi kutokana na stendi hiyo kujaa maji na tope wakati wa masika. Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya Karagwe bwana Wallece Mashanda…
27 April 2021, 5:55 pm
DC Mwilla ashiriki kuondoa maji kwenye makazi ya watu
Baada ya nyumba kadhaa na barabara za mitaa kujaa maji kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha Wilayani Missenyi, leo April 27,2021 Mkuu wa Wilaya Missenyi Kanali Denisi Mwila ameshirikiana na wananchi kuzibua mitaro na mifereji ya maji iliyoziba nakusababisha maji kujaa…
27 April 2021, 12:02 pm
Timu ya Nyaishozi SC kutua Bungeni wiki hii
Na Shabani Ngarama, Karagwe FM Timu ya Nyaishozi kutoka wilaya ya Karagwe iliyowakilisha mkoa wa Kagera kwa kupanda daraja la pili katika michuano ya fainali ya ligi za mikoa iliyofanyika mkoani Lindi imepata fursa ya kupumzika Dodoma wakati ikitokea mkoani…
26 April 2021, 8:20 pm
Wakosa makazi kwasababu ya Mafuriko.
Mvua zinazoendelea kunyesha katika sehemu mbalimbali Wilayani Missenyi zimesababisha baadhi ya barabara za mitaa na makazi ya watu katika mji mdogo wa Kyaka Bunazi kujaa maji huku baadhi ya wakazi wa mji huo wakilazimika kuhama makazi Mkuu wa Wilaya Missenyi…
24 April 2021, 7:28 am
Halmashauri zote zapewa maagizo.
Mkuu wa mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco Gaguti amewataka wajasiriamali wadogo kuchangamkia fursa ya kupata vitambulisho vipya vya kielectroniki vilivyoanza kutolewa na mamlaka ya mapato Tanzania TRA. Ametoa wito huo wakati alipokuwa akiongea na wakuu wa wilaya pamoja na…
20 April 2021, 9:26 am
Jeshi la zimamoto laungana na Skauti kukabili moto.
Jeshi la zimamoto na uokoaji wilayani Karagwe limeungana na Skauti wilayani humo ili kuongeza nguvu katika kukabiliana na majanga ya moto ambayo yamekuwa yakiteketeza mali za watu na kuwarudisha nyuma kimaendeleo. Staff Sergeant Peter Mbale ni Kamanda wa Jeshi la…
19 April 2021, 4:32 pm
Sekondari 15 kati ya 22 zafanikisha Lishe
Afisa Elimu sekondari wilayani Missenyi mkoani Kagera Mwl Saverina Misinde amezipongeza shule za sekondari 15 za serikali zinazotoa huduma ya chakula cha mchana ili kuwawezesha wanafunzi kujifunza vizuri wakiwa wameshiba Pongezi hizo amezitoa hivi karibuni wakati Kamati ya fedha Utawala…
17 April 2021, 5:21 pm
Wananchi walia na ubovu wa Barabara.
Wananchi wa kitongoji cha Karundu kata ya Bugene wilaya ya Karagwe mkoani Kagera wameiomba Halmashauri ya wilaya Karagwe iwatengenezee barabara za kitongoji hicho kwani wao wamejitolea bila kupata msaada mpaka wamechoka. Wananchi hao wamebainisha kero hiyo wakiwa kwenye mkutano wa…
16 April 2021, 9:32 pm
Kitendawili chateguliwa Kyenjubu.
Wananchi walionunua viwanja eneo la Kyenjubu Missenyi Mkoani Kagera wako mbioni kukabidhiwa viwanja vyao ili waviendeleze Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Missenyi Innocent Mukandala amesema kuwa shughuli yakutengeneza barabara iliyokuwa imekwamisha zoezi lakukabidhi wananchi viwanja vyao inaendelea vizuri nakwamba…