Karagwe FM

Recent posts

26 May 2021, 7:07 pm

Wapewa saa 48 kuhamisha vibanda.

Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya Karagwe Godwin Kitonka amewataka wajasiriamali wanaofanya biashara katika stendi ya Kayanga wilaya Karagwe kuhamisha vibanda vilivyojengwa katika eneo hilo kabla ya May 27 mwaka huu. Bwana Kitonka ametoa kauli hiyo Mei 26 mwaka huu…

18 May 2021, 8:59 pm

Watuhumiwa wa wizi wafyekewa Migomba na kubomolewa Nyumba.

Wananachi wenye hasira kali katika kijiji cha Rukole kata Ihanda wilaya ya Karagwe mkoani Kagera wamevamia na kubomoa nyumba pamoja kufyeka migomba ya wananchi wa kitongoji cha Kalalo wanaotuhumiwa kujihusisha na vitendo vya uhalifu kijijini humo. Akizungumuza katika eneo la…

17 May 2021, 10:16 pm

Watano watumbuliwa Misenyi

Viongozi 5 wa Chama Cha Ushirika wa wakulima wa miwa Missenyi UWAMMISE na BUBARE AMCOS wameondolewa kwenye uongozi baada yakukiuka kanuni na taratibu za Ushirika. Akitangaza kuwaondoa kwenye uongozi Jumatatu Mei 5 mwaka huu ,Afisa Ushirika Wilaya ya Missenyi Gabinus…

12 May 2021, 3:35 pm

Ulinzi kuimarishwa wakati wa Eid.

Jeshi la Polisi wilaya ya Karagwe mkoa wa Kagera  limeanzisha doria maalumu kwaajili ya kupambana na vitendo vya uharifu na kuimarisha usalama wakati wa sikukuu ya Eid EL Fitri. Henry Benard Makwasa ni Mkuu wa Jeshi la Polisi wilaya ya…

11 May 2021, 12:01 pm

Waziri Bashungwa awafuturisha Waislamu.

Mbunge wa jimbo la Karagwe Innocent Bashungwa ambaye pia ni waziri wa habari,utamaduni sanaa na michezi amewafuturisha waumini wa dini ya kiislamu pamoja na wageni waalikwa huku Futari hiyo ikiambatana na harambee ya ujenzi wa kituo cha afya. Shehe wa…

11 May 2021, 11:34 am

Miradi yalamba Milioni 96 kwa miezi 3.

Zaidi ya shilingi Milioni 96 zimetumika kutekeleza miradi mbalimbali ya kimaendeleo katika kata ya Kayanga wilaya Karagwe kwa kipindi cha robo ya mwaka 2021. Akizungumza na Redio Karagwe Fm sauti ya wananchi May 11 mwaka huu,Diwani wa kata Kayanga bwana…

5 May 2021, 2:40 pm

Bilakwate: Gongo iruhusiwe Kagera

Mbunge wa jimbo la Kyerwa mkoani Kagera Innocent Bilakwate ameiomba serikali kuruhusu pombe ya moshi au Gongo inayotokana na ndizi kali maarufu kama “ENKONYAGI au KARIINYA” akidai kuwa pombe hiyo ni halali kwa sababu inatokana na ndizi ambazo ni chakula…

4 May 2021, 11:09 am

Shilingi milioni 626 kukarabati shule wilayani Karagwe

Halmashauri ya wilaya Karagwe imepokea shilingi milioni 626 kwa ajili ya ukarabati na ujenzi wa miundombinu katika baadhi ya shule za msingi na Sekondari wilayani Karagwe mkoani Kagera. Taarifa hiyo imetolewa na mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Karagwe Wallace…

2 May 2021, 12:59 pm

World Vision Tanzania Kanda ya Kagera yatoa faraja Missenyi

Shirika la World Vision Tanzania Kanda ya Kagera mradi wa Missenyi limekabidhi msaada wa vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni 12.5 kwa zaidi ya watu 300 wanaoishi kwenye kambi baada ya kuhama makazi yao Akikabidhi msaada huo kwa Mwenyekiti wa…

1 May 2021, 7:09 pm

Chanzo cha maji Katoke hatarini kutoweka

Chanzo cha maji cha Katoke kilichopo katika kitongoji cha Ruzinga kata ya Bugene wilayani Karagwe,kipo hatarini kutoweka kutokana na baadhi ya wafugaji wa ng`ombe kukigeuza kuwa eneo la kunyweshea mifugo yao. Wakazi wa kitongoji hicho wameieleza Radio Karagwe Sauti ya…

KARAGWE FM PROFILE

UTANGULIZI.
Radio Karagwe ni Radio ya kijamii iliyoanzishwa na shirika lisilokuwa la kiserikali lijulikanalo kama Karagwe Media Association (KAMEA).Ilianza kurusha matangazo yake Desemba 11.2007 kupitia masafa ya 91.4 MHz kwa ufadhili wa shirika la nchini Denmark (ULD80 Karagwe Venor) waliowezesha mafunzo kwa watumishi na upatikanaji wa vifaa.

DIRA.
Kuziba pengo la mawasiliano kwa wananchi wa Karagwe ambao kwa wakati huo hawakuwa na uwezo wa kusikiliza radio za Tanzania kutokana na jiongrafia ya eneo.

MAENEO REDIO INAKOSIKIKA
Kwa mujibu wa utafiti uliofanywa na ULD80 June mwaka 2012 Radio Karagwe ina zaidi ya wasikilizaji milioni 1.2.(KM 200 KUTOKA MAKAO MAKUU).Inasikika katika maeneo mbalimbali ya mkoa wa Kagera,katika wilaya za Karagwe, Kyerwa, Missenyi, Muleba na Bukoba Vijijini. Inasikika katika maeneo machache wilaya za Ngara, Biharamulo na Bukoba manispaa. Pia inasikika maeneo ya nchi jirani za Uganda, Burundi na Rwanda.

MAWASILIANO.
S.L.P 316,KARAGWE KAGERA TZ
E-mail : radiokaragwe@gmail.com
Phone: +255 754 677 708 / +255 689 471 171