Karagwe FM

Halmashauri ya Missenyi yapitisha bajeti ya shilingi bilioni 56.8

4 March 2026, 8:00 pm

Mwenyekiti wa halmashauri ya Missenyi Phocas Rwegasira. Picha na Respicius John

Baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya ya Missenyi mkoani Kagera limeridhia kukusanya na kutumia kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 56.8 kwa mwaka wa fedha ujao.

Na Respicius John, Missenyi

Baraza la madiwani la halmashauri ya wilaya missenyi limepitisha zaidi ya shilingi bilioni 56.8 kwa ajili ya mpango na bajeti ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha 2026/2027.

Bajeti hiyo imepitishwa na baraza hilo baada ya mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Missenyi Phocas Rwegasira kuwahoji madiwani wakati wa kikao cha bajeti kilichoketi katika ukumbi wa halmashauri Machi 4. 2026 ambao kwa pamoja wameridhia kupitishwa kwa bajeti hiyo.

Hata hivyo amewaomba wadau mbalimbali kushirikiana na halmashauri katika kufanikisha ufanisi wa bajeti hiyo

Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Missenyi Phocas Rwegasira
Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Missenyi John Paul Wanga. Picha na Respicius John

Awali akiwasilisha rasimu ya mpango na bajeti kwa ajili ya mwaka wa fedha 2026/2027 mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Missenyi bw. John Paul Wanga ameliomba baraza kuidhinisha kiasi cha zaidi ya shilingi bilioni 56.8

Mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya wilaya ya Missenyi bw. John Paul Wanga
Baadhi ya madiwani wakiwa wamesimama wakati mwenyekiti akiondoka ukumbini baada ya mkutano

Baadhi ya madiwani akiwemo Aspon Mwijage na Walter Nyahoza wameishauri halmashauri hiyo kukamilisha miradi viporo sambamba na kuimarisha ukusanyaji wa mapato ya ndani huku diwani wa kata ya Kyaka Jawili Twahili akishukuru kupangiwa fedha za miradi katika kata yake

Baadhi ya madiwani wakitoa maoni yao