Karagwe FM
Karagwe FM
1 October 2025, 8:10 am

“Mwaarobaini wa soko la kahawa jimbo la Karagwe ni kufuta vyama vya ushirika na kuongeza thamani ya zao hilo kwa kujenga viwanda kila kata”…Anasema Mhina
Na Shabani Ngarama, Karagwe, Kagera
Mgombe ubunge jimbo la Karagwe Bw. Rwegasira Hemed Mhina ameahidi kuboresha maisha ya wakulima wa kahawa kwa kufuta vyama vya ushirikia akidai kuwa vimekuwa chanzo cha umasikini wa mkulima
Akiwa katika mkutano wa kampeni uliofanyika Septemba 30.2025 eneo la maegesho ya magari madogo kwa Musukuma Omurushaka kata ya Bugene wilayani Karagwe mkoani Kagera Mhina ametaja vipaumbele kadhaa ikiwa ni pamoja na kuanzisha viwanda kata zote za wilaya ya Karagwe kama sehemu ya kuongeza thamani ya kahawa na kukuza uchumi

Pamoja na kuboresha maslahi ya wakulima wa kahawa Bw. Mhina ameahidi kutatua changamoto ya miundombinu ya barabara, afya, maji na elimu akisisitiza kuwa atachochea upatikanaji wa ajira kwa vijana wanaohitimu elimu ya juu

Awali akijibu maswali yaliyogusia kero za wananchi aliwataka wananchi hao kuwachagua wagombea wa udiwani kupitia ACT Wazalendo ili wawe chache ya mabadiliko kupitia baraza la madiwani ndani ya halmashauri ya wilaya ya Karagwe
Kata zenye wagombea udiwani wa chama cha ACT Wazalendojimbo la Karagwe ni Rugu, Ihembe, Nyaishozi, Kibondo, Igurwa na Kihanga kati ya kata 23 za halmashauri ya wilaya ya Karagwe