Karagwe FM
Karagwe FM
26 September 2025, 11:37 am

Shirika la CBIDO lenye makao makuu yake wilayani Karagwe limeendelea na mradi wake wa Pamoja unaolenga kuzuia ulemavu na kutoa huduma za utengamao kwa watu wenye ulemavu kwa kata za Kyaka na Kilimilile Wilayani Missenyi mkoani Kagera na mara hii likitoa msaada wa vifaa tiba
Na Respicius John, Missenyi, Kagera
Zahanati za Kyaka na Kilimilile zilizoko wilayani Missenyi zimepokea msaada wa mashine ya mionzi ultra sound kutoka shirika la CBIDO la Karagwe itakayosaidia kuchunguza wanawake wajawazito ili kudhibiti ulemavu kwa watoto kabla ya kuzaliwa

Akikabidhi mashine na kitanda chake vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 14 meneja miradi wa shirika la CBIDO Bw. Donatus Kaihura amesema kuwa mashine hiyo imetolewa kama sehemu ya utekeleza wa mradi wa kuzuia ulemavu na kutoa huduma za utengamao ambapo kaimu mganga mkuu wa halmashauri ya Missenyi Dkt Jamil Yahya ametoa shukurani kwa shirika hilo
Nao baadhi ya wataalam wa afya katika zahanati za Kilimilile na Kyaka wamesema kuwa mashine hizo zitasaidia pakubwa katika kupunguza matatizo ya uzazi kwa wananchi
Baadhi ya wanufaika wa kike na kiume wameeleza kufurahishwa kwao na msaada huo kwenye maeneo yao wakisema kuwa kimesaidia kurahisha huduma za uzazi