Karagwe FM

SHIVYAWATA Bukoba yapongeza utumishi wa Lugangila

8 August 2025, 7:52 pm

Baadhi ya viongozi wa SHIVYAWATA Bukoba wakiwa katika picha ya pamoja. Picha na Theophilida Felician

Viongozi wa shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu SHIVYAWATA katika manispaa ya Bukoba mkoani Kagera wameonesha kutoridhishwa na kura za maoni za wajumbe wa chama cha mapinduzi CCM zilizomnyima ushindi aliyekuwa mbunge wa mashirika yasiyokuwa ya kiserikali Neema Lugangila huku wakianika mchango wake kwa shirikisho hilo

Na Theophilida Felician, Bukoba.

Viongozi wa Shirikisho la vyama vya watu wenye ulemavu Tanzania SHIVYAWATA manispaa ya Bukoba mkoa Kagera wameshukuru na kupongeza mchango wa aliye kuwa mbunge wa viti maalum kupitia asasi za kiraia NGOs Neema Lugangira kwa namna alivyokuwa karibu na kundi la watu wenye ulemavu mkoa Kagera.

Mwenyekiti wa chama cha wasioona TLB mkoa wa Kagera Annalise Lubago. Picha na Theophilida Felician

Baadhi ya viongozi hao wakiwa ofisini kwao maeneo ya ofisi ya mkuu wa mkoa wa Kagera wakiongozwa na mwenyekiti wa chama cha wasioona TLB mkoa Annalise Lubago wamesema Neema akiwa katika uongozi hakuwasahau bali alishirikiana nao mambo tofau hususan kuwashika mkono pale walipokuwa na uhitaji wa vitu muhimu.

Mwenyekiti wa chama cha wasioona TLB mkoa wa Kagera Annalise Lubago
Mwenyekiti SHIVYAWATA manispaa ya Bukoba bw. Novati Joseph Mwijage. Picha na Theophilida Felician

Mwenyekiti SHIVYAWATA manispaa ya Bukoba bw. Novati Joseph Mwijage amefafanua kuwa mchango wa mbunge huyo uliwagusa kama kundi, mtu mmoja mmoja jambo lililowatia faraja ambapo pia viongozi hao kwa pamoja wameyataja mengi likiwemo tukio la kuwanunulia ng’ombe na kumpeleka ofisini kwao kwa ajili ya kitoweo Juni 14. 2025 kama wanavyobainisha Jackline Asimwe Fabian kutoka Chama cha watu wenye ulemavu CHAWATA manispaa ya Bukoba.

Jackline Asimwe Fabian na Novati Joseph Mwijage

Wamehitimisha wakimuombea heri katika majukumu yake kwani ni mpambanaji kupitia njia mbalimbali huku wakimsihi kutokata tamaa baada ya kura za maoni kuwania nafasi hiyo ya ubunge awamu nyingine kushindwa kutosha.