Karagwe FM
Karagwe FM
26 May 2025, 7:12 pm

Vijana mkoani Kagera wameaswa kukaa kando na makundi ya kisiasa yanayotumia kundi hilo kuleta vurugu nyakati za uchaguzi
Na, Theophilida Felician, Bukoba.
Kuelekea uchaguzi mkuu vijana mkoani Kagera na Tanzania kwa ujumla wametakiwa kuwa makini na watu wenye nia ya kuwashawishi kushiriki matendo ya vurugu za kuhatarisha amani ya nchi.
Wito huo umetolewa na viongozi wa taasisi ya mabalozi wa amani Tanzania PPA yenye makao yake manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.
Wakizungumza na vyombo vya habari viongozi hao wamefafanua kuwa nyakati kama hizi kundi la vijana huonekana kama kundi muhimu hivyo hujikuta wakitumiwa na watu mbalimbali wakiwemo wanasiasa kwa malengo ya kuwavusha katika harakati zao za kisiasa na wengine huwatumia ndivyo sivyo hali inayosababisha kuwepo kwa matukio ya vurugu
Maulid Rashidi Kambuga ni mkurugenzi wa taasisi hiyo ambaye amesema amani ikishatoweka hakuna pa kukimbilia iwe kwa vijana, wazee, akina mama, watoto wote wanaathirika.

Naye Mchungaji Clavery Venant ambaye ni mkurugenzi msaidizi wa PPA amebainisha kuwa kundi la vijana hawana budi kuishi kwa hofu ya Mungu na kuzingatia misingi ya maadili mema huku Bahati Ildephonce ambaye ni mkazi wa Bukoba yeye akieleza kuwa amani ikishavunjika husababisha madhara mengi kwa jamii

Kwa pamoja wametoa wito kwa wananchi kuwa wazalendo wa kweli ili kulinda na kujenga Tanzania ya amani kwani