Karagwe FM
Karagwe FM
18 February 2025, 8:06 pm

Wafanyabiashara na wajasiriamali nchini wameendelea kukumbwa na hasara za mara kwa mara kutokana na moto unaoripuka katika maeneo yao ya kazi kutokana na uhaba wa miundombinu rafiki ya uzimaji moto pindi unapotokea
Na Respicius John
Wafanyabiashara katika mji mdogo wa Bunazi wilayani Missenyi wamepata hasara baada ya moto kuteketeza jumla ya vibanda kumi pamoja na mali zote zilizokuwemo ambazo thamani yake haijajulikana
Kwa mujibu wa mwenyekiti wa kitongoji cha Kashozi B kata ya Kasambya wilayani Missenyi Mwl. Ruchius Bukambu vibanda hivyo viliunguzwa na moto ulioripuka usiku wa kuamkia Februari 17.2025

Mmoja wa wafanyabiashara waliokuwa na vibanda katika eneo hilo bi Edina Josia amesema kuwa alipokea simu ya saa 7:30 usiku akitaarifiwa kuungua kwa eneo la biashara zao na kwamba alipofika alikuta kila kitu kikiwa kimeteketea huku mashuhuda wakisema kuwa huenda moto huo ulitokana na hitilafu ya umeme
Hata hivyo kaimu kamanda wa jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa Kagera Joseph Ngonyani amesema kuwa chanzo cha moto bado kinachunguzwa na kwamba hakuna madhara ya kibinadamu yaliyojitokeza