Karagwe FM

Mbunge wa Nkenge Missenyi asimulia alivyonusurika katika ajali

6 December 2024, 9:12 pm

Mbunge wa jimbo la Nkenge wilaya ya Missenyi mkoani Kagera bw. Florent Kyombo

Wabunge 16 wakiwemo wawili wa mkoa wa Kagera Florent Kyombo wa Nkenge na Innocent Bilakwate wa Kyerwa, maofisa wawili wa bunge na dereva wa basi la kampuni ya mabasi ya Shabby wamejeruhiwa katika ajali ya gari iliyotokea eneo la Mbande, Wilayani Kongwa mkoani Dodoma.

Na Respicius John, Shabani Ngarama

Mbunge wa jimbo la Nkenge wilaya ya Missenyi mkoani Kagera amesema kuwa ajali ya basi lililobeba wabunge waliokuwa wakielekea Mombasa nchini Kenya imetokea wakiwa katika msafara wa mabasi manne yeye akiwa katika basi namba 3 lililopata ajali wakienda nchini Kenya kwenye mashindano ya michezo

Akiongea na Radio Karagwe akiwa katika wodi baada ya ajali hiyo bw. Kyombo amewashukuru wananchi wanaoendelea kumuombea na kuwahakikishia kuwa anaendelea vizuri licha ya majeraha aliyoyapa kwenye ajali hiyo

Sauti ya mbunge wa Nkenge Florent Kyombo

Ameongeza kuwa ajali ilikuwa kubwa licha ya kwamba wote walioumia wanaendelea kuimarika na kuwasisitiza wananchi kumuombea yeye na wabunge wengine ili warejee katika hali zao za kawaida