Karagwe FM

Upepo waacha kaya 73 bila makazi Muleba

6 November 2024, 11:30 am

Moja ya nyumba zilizoezuliwa na upepo katika kijiji cha Kibungu A kata ya Katoke wilayani Muleba. Picha na Shafiru Yusuph Athumani

Vipindi vya mvua zinazoambatana na upeo mkoani Kagera zimekuwa zikisababisha madhara mbalimbali kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kuezua nyumba na kuwaacha bila makazi sambamba na kuharibu baadhi ya mazao mashambani

Na Jovinus Ezekiel

Kaya 73 zimeathiriwa na upepo mkali katika kijiji cha Kibungu A kata ya Katoke wilayani Muleba ikiwemo kuezua mabati ya nyumba 11 na kusababisha baadhi ya wananchi kukosa mahala pa kuishi.

Sehemu ya shamba la migomba na mihogo lililoathiriwa na upepo. Picha na Shafiru Yusuph Athumani

Akizungumza baada ya kushuhudia uharibifu uliosababishwa na upepo mkali diwani wa kata ya Katoke bw. Eliud Mkwenda amesema kuwa mbali na kaya 73 kuathiriwa kwa kukosa mahala pa kuishi upepo huo uliovuma majira ya saa saba mchana wa Novemba 4, 2024 pia umesababisha uharibifu wa mazao kama migomba, kahawa, mahindi na mihogo na kuwaomba wadau mbalimbali kusaidia kaya zilizopata madhara hayo

Sauti ya diwani wa kata ya Katoke wilayani Muleba bw. Eliud Mkwenda

Kwa upande wao baadhi ya wananchi waliopata madhara ya upepo huo bw.Hamza Elias na bi Grace Sosthenes wamesema kuwakwa sasa hawana malazi wala chakula kwa kuwa mali zao zimeharibika na kwa sasa wanaishi kutokana na msaada wa majirani

Sauti za wananchi bw.Hamza Elias na bi Grace Sosthenes
Moja ya nyumba zilizoezuliwa na upepo katika kijiji cha Kibungu A kata ya Katoke wilayani Muleba. Picha na Shafiru Yusuph Athumani