Karagwe FM

RC Kagera kula sahani moja na wahamiaji haramu

9 October 2024, 10:18 pm

Rc Kagera hajat Fatma Mwassa akiongea na vyombo vya habari.Picha na Theophilida Felician

Uhamiaji haramu una athari kubwa kwenye soko la ajira mkoani Kagera.Wahamiaji wasio na nyaraka mara nyingi hufanya kazi katika sekta za kilimo, ujenzi, na ufugaji ambapo kuna mahitaji ya ajira, na waajiri huwatumia kwa gharama ndogo huku wazawa wakikoswa ajira

Theophilida Felician

Kauli hiyo imetolewa naye mkuu wa mkoa Kagera hajat Fatma Mwassa wakati akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake manispaa ya Bukoba.

Amesema zoezi la uandikishaji litaanza Tarehe 11 Oktoba hadi 20, 2024 na uchaguzi ni Tarehe 27 Novemba.

Rc Kagera hajat Fatma Mwassa akizungumzia wahamiaji kutoruhusiwa kugombea katika uchaguzi ujao

Amefafanua kuwa mkoa Kagera unakadiliwa kuwa na watu wenye umri wa miaka18 na kuendelea wapatao 1,566,530 ambapo kati hao wanaume ni 750, 003 na wanawake 816527.

amesema kuwa vituo vya uandikishaji wapiga kura vipatavyo 3833 vimeandaliwa mkoani Kagera na zoezi la kuchukua na kurejesha fomu litafanyika Tarehe 1 hadi 7 Novemba na kampeni zitafanyika kuanzia Tarehe 20 hadi 26 Novemba 2024 amesema mkuu wa mkoa Fatma Mwassa.

Rc Kagera hajat Fatma Mwassa akitoa ufafanuzi zaidi wakati akiongea na waandishi wa habari

Ametoa wito kwa wagombea wa vyama vya siasa kutumia muda huo vizuri kwa kufanya kampeni za kistaarabu ili kuhakikisha uchaguzi unafanyika kwa amani na utulivu huku akiwasisitiza wananchi kujitokeza na kushiriki uchaguzi huo kikamilifu.

Rc Kagera hajat Fatma Mwassa akizungumzia swala la kampeini za kistaarabu

Hata hivyo Amelezea juu ya maadhimisho ya siku ya chakula duniani ambapo kitaifa yatafanyika mkoani Kagera kuanzia mnamo tarehe 10 Oktoba na kuhitimishwa 16, 2024 katika viwanja vya CCM manispaa ya Bukoba.

Rc Kagera hajat Fatma Mwassa akizungumzia maadhimisho ya siku ya chakula duniani

Amewakaribisha wananchi wote wa Kagera na kwingineko kujitokeza ili kujionea mambo mbalimbali yatakayofanyika katika maadhimisho hayo muhimu.

Rc Kagera Fatma Mwassa akizungumza na waandishi wa habari mkoa Kagera.Picha na Theophilida Felician