Karagwe FM

KDCU Ltd yatumia shilingi milioni 500 ujenzi wa ghala Karagwe

26 June 2024, 11:49 am

Chama kikuu cha ushirika cha wilaya za Karagwe na Kyerwa mkoani Kagera KDCU Ltd kimekuwa na harakati za mara kwa mara kwa ajili ya kujenga ushirika imara unaowanufaisha wakulima wa kahawa na kujiimarisha kiuchumi kupitia mbinu mbalimbali, na mara hii wameamua kuwekeza katika ujenzi wa ghala jipya la kuhifadhia kahawa ili kuwawezesha wakulima kupata hifadhi ya zao hilo kwa usalama zaidi.

Na Ospicia Didace

Mrajis wa vyama vya ushirika Tanzania bara Dkt Benson Otieno Ndiege ameweka jiwe la msingi kwenye ghala la kuhifadhia kahawa la chama kikuu cha ushirika cha wilaya za Karagwe na Kyerwa mkoani Kagera KDCU Ltd katika eneo la Kamahungu kata ya Kayanga ambalo mpaka sasa limegharimu zaidi ya shilingi milioni 400 na kupongeza mfumo wa kahawa unaotumika kwa sasa kwani unamjali mkulima.

Jiwe la msingi la ujenzi wa ghala la mazao Kamahungu, Kayanga wilaya ya Karagwe. Picha na Ospicia Didace

Baada ya kuweka jiwe la msingi mrajisi wa vyama vya ushirika Tanzania Bara dkt Benson Otieno Ndiege amewapongeza KDCU Ltd kwa kuwekeza katika ujenzi wa ghala hilo ambalo mpaka linakamilika litagharimu zaidi ya shilingi milioni 500 akisema kuwa ushirika lengo lake ni kuwaunganisha watu pamoja na kupata manufaa ya mazao wanayozalisha.

Sauti ya Mrajis wa vyama vya ushirika Tanzania bara Dkt Benson Otieno Ndiege

Kwa upande wake kaimu meneja mkuu wa KDCU Ltd bw.Domitian Robart Kigunia akisoma risala fupi mbele ya mgeni rasmi amesema ujenzi wa ghala hilo unalenga kuhifadhi vizuri kahawa na kuzitunza vizuri likiwa limefikia zaidi ya aslimia 80 na ujenzi utakuwa umekamilika ndani ya wiki mbili kuanzia sasa.

Sauti ya kaimu meneja mkuu wa KDCU Ltd bw.Domitian Robart Kigunia
Mrajis wa vyama vya ushirika Tanzania bara Dkt Benson Otieno Ndiege (aliyesimama). Picha na Ospcisia Didace

Pamoja na hayo Mrajis Ndiege amesema KDCU Ltd imekuwa mfano mzuri kwenye uwekezaji akisema kuwa ushirika ni lazima kuongeza thaman ya kile kidogo kinachopatikana.

Sauti ya mrajis wa vyama vya ushirika Tanzania bara Dkt Benson Otieno Ndiege
Mwenyekiti wa chama kikuu cha ushirika wilaya za Karagwe na Kyerwa KDCU Ltd Fackson Josiah (aliyesimama). Picha na Ospicia Didace

Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama kikuu cha ushirika wilaya za Karagwe na Kyerwa KDCU Ltd Fackson Josiah ameishukru serikali chini ya Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kwa kuanzisha mfumo mpya wa uuzaji wa kahawa akisema umekuwa mkombozi kwa mkulima.

Sauti ya mwenyekiti wa chama kikuu cha ushirika wilaya za Karagwe na Kyerwa KDCU Ltd Fackson Josiah

Imeelezwa kuwa Ushirika ni chachu na lengo ni  kuwaunganisha watu kupata bei nzuri na kinachotekelezwa ni maono ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambapo amewataka viongozi wa vyama vya msingi wanapata semina elekezi ili kuwawezesha kupata hati safi.