Tume ya haki za binadamu yahimiza ulinzi wa haki kwa wote Bukoba
12 June 2024, 6:11 pm
Suala la ulinzi wa haki za binadamu ni miongoni mwa mambo yasiyopewa kipaumbele na jamii wakiamini kuwa ni jukumu la kundi au watu maalumu.
Na Theophilida Felician
Kamishna wa Tume ya Haki za Binadamu na utawala bora bw. Nyanda Shuli amewaasa wananchi wa manispaa ya Bukoba mkoani Kagera kuwajibika katika suala la kulinda haki za binadamu.
Ametoa kauli hiyo Juni 12, 2024 wakati akiwahutubia wakazi wa manispaa ya Bukoba kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika katika mtaa wa Uhuru kata ya Bilele na kuongeza kuwa njia ya kuzilinda haki ni pamoja na kutoa taarifa pale mtu anapoona haki ya mtu inakanyagwa hususani zile za kijamii.
Amefafanua kwamba licha ya kuwepo wajibu kwa serikali kuzilinda na kuhakikisha kuna mifumo inayowahakikishia wananchi haki hizo pia zinatazama namna wananchi wanavyotendeana huko wanakoishi.
Hata hivyo ameongeza kusema kuwa tume hiyo imeundwa kwa mjibu wa katiba ili kusaidia nakuwezesha utetezi ,ufuatiliaji na ulinzi wa haki za binadamu na misingi ya utawala bora ambayo umewekwa ngazi tofauti tofauti ikiwemo mahakama na ofisi mbalimbali za serikali zinazowahudumia wananchi.
Amehitimisha akisema kuwa tume ya haki za binadamu ni idara huru ya serikali iliyoanzishwa kama taasisi yakitaifa iliyo na kitu chakukuza na kulinda haki za binadamu na utawala bora nchini, imepewa nguvu na katiba pamoja na Sheria kwa malengo ya kuwahudumia wananchi pale wanapokuwa na mkwamo katika ufutaliaji haki huku akiwasihi wananchi kutokusita kuifikia tume hiyo pale wanapokwama maeneo mengine ya utoaji haki.
Constantine Mugusi ambaye ni afisa uchunguzi mkuu katika tume hiyo amesema kuwa kwa mujibu wa miongozo ya dunia ni tume ya haki za binadamu pekee iliyopewa jukumu la kuihoji serikali pale mambo ya haki yanapokuwa yamekiukwa huku akizitaja baadhi
Kwa upande wake diwani wa kata ya Bilele Tawfiq Sharif Salum amepongeza ujio wa tume hiyo Bukoba na kuwafikia wananchi kwa kuwapatia elimu stahiki ya haki za binadamu.
Ameiomba tume kuanzisha ofisi Mkoani Kagera ili wananchi waweze kunufaika kwa ukaribu huduma hiyo badala ya kuifuata mkoani Mwanza kutokana na umbali uliopo na hali yao kiuchumi.