Karagwe FM

RUWASA Missenyi yalalamikia uhujumu wa miundombinu

12 June 2024, 10:15 am

Baadhi ya wakazi wa kata ya Ruzinga wilayani Missenyi wamelalamikiwa na mamlaka ya maji na usafi wa mazingira vijijini RUWASA kwa kuhujumu miundombinu ya mradi wa maji ruzinga kwa kukata mabomba ya maji.

Katika taarifa upatikanaji wa maji wilayani Missenyi iliyosomwa na Mussa Masorwa kwa niaba ya meneja wa RUWASA wa wilaya kwa wajumbe wa kamati ya lishe ya wilaya imeeleza kuwa baadhi ya wananchi wa kata ya Ruzinga wilayani humo wanahujumu miundombinu ya mradi wa maji kwa kukata mabomba

Sauti ya kaimu meneja wa RUWASA wilaya ya Missenyi bw. Mussa Masorwa. Picha na Respicius John

Hata hivyo tuhuma za wananchi wa Ruzinga kuhujumu mradi wa maji diwani wa kata hiyo Rafiu Hussein amesema kuwa RUWASA wanawasingizia wananchi ili kupata pa kutokea kutokana na kushindwa kwao kutoa huduma kwa wananchi.