Karagwe FM

Serikali mbioni kujenga uwanja wa ndege Omukajunguti Missenyi

30 May 2024, 5:35 pm

Mkuu wa mkoa wa Kagera Hajat Fatma Mwasa akihutubia madiwani wa halmashauri ya Missenyi. Picha na Respicius John

Kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa nchini na duniani, uwanja wa ndege wa Bukoba umekuwa na changamoto ya kugubikwa na mawingu hali inayoleta adha kwa marubani na abiria mara kwa mara ukiachilia mbali ajali ya ndege ya kampuni ya Precision iliyotumbukia Ziwa Victoria mwishoni mwa mwaka 2022. Hali hii imesababisha baadhi ya wanaharakati na wanasiasa kuiomba serikali kujenga uwanja wa ndege mpya mkoani Kagera eneo la Omukajunguti.

Na Respicius John

Mkuu wa mkoa wa Kagera Hajat Fatma Mwasa amesema kuwa serikali itaanza upembuzi yakinifu kwa ajili ya ujenzi wa uwanja wa ndege Omukajunguti wilayani Missenyi mkoani Kagera katika bajeti ya mwaka wa fedha unaoanza mwezi Julai mwaka huu

Amesema hayo wakati akihutubia baraza la madiwani Missenyi lililoketi kwa ajili ya kujadili hoja za mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali CAG katika ukumbi wa William F.Katunzi halmashauri ya wilaya ya Missenyi

Sauti ya mkuu wa mkoa wa Kagera Hajat Fatma Mwasa akihutubia madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Missenyi
Mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Missenyi Projestus Tegamaisho (aliyesimama kulia).
Picha na Respicius John

Akiongea katika baraza hilo Mwenyekiti wa halmashauri ya Missenyi ambayo kwa mujibu wa ripoti ya mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali imepata hati safi kwa mara ya 8 mfululizo mwenyekiti wa halmashauri hiyo Projestus Tegamaisho amemuomba mkuu wa mkoa kuwaongezea bajeti ya miundombinu ya barabara sambamba na kumuahidi ongezeko la mapato kupitia miradi ya kimkakati.

Sauti ya mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Missenyi Projestus Tegamaisho