DAS Karagwe akabidhi misaada ya Rais Samia kwa makundi maalum
16 April 2024, 8:10 am
Imekuwa desturi ya viongozi wakuu wa serikali na mashirika ya umma na binafsi kutoa zawadi za sikukuu za kidini kama Krismas, Mwaka mpya, Pasaka na hata Eid El fitri na eid el addha kwa ajili ya kuwezesha makundi maalum kufurahia sikukuu kama watu wengine
Katibu tawala wilaya ya Karagwe (aliyevaa kanzu na kofia kulia) Rasul Eliud Shandala akikabidhi msaada wa vyakula na vinywaji kwa mkurugenzi wa shirika lisilokuwa la kiserikali TOSO bi Aines Samweli (anayetabasamu kushoto akishikilia kamba ya mbuzi) linalohuduma watu wenye mahitaji maalum. Picha na: Thomas Ntobi-Afisa habari wa halmashauri ya wilaya ya Karagwe
Na Ospicia Didace
Vijana na watoto wanaosoma ufundi katika kituo cha watoto yatima TOSO katika kata ya Kayanga wilayani Karagwe wamenufaika na msaada wa mahitaji ya sikukuu ya eid el fitri kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan kupitia ofisiya mkuu wa wilaya ya Karagwe.
Akikabidhi zawadi hizo kwa niaba ya Rais Samia hivi karibuni katibu tawala wa wilaya ya Karagwe bw. Rasul Eliud Shandala aliyemwakilisha mkuu wa wilaya ya Karagwe bw.Julius Laizer akiambatana na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Karagwe Dr. Amon David Mkoga na baadhi ya wataalamu wa halmashauri hiyo amewataka wazazi kutowabagua na kuwanyanyasa watoto wenye ulemavu na badala yake wawape mahitaji ya msingi sawa na watoto wengine
Sauti ya katibu tawala wilaya ya Karagwe Rasul Eliud Shandala
Kwa upande wake mkurugenzi wa kituo cha watoto yatima TOSO wilaya ya Karagwe AINES Samwel amemshuru Rais Samia kwa msaada huo na kutoa wito kwa wadau wengine wa maendeleo kuiga mfano wa Rais wa kula sikukuu na wenye mahitaji wakiwemo yatima
Bw.Shandala aliyemwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Karagwe Julius Kalanga Laiser ambaye yupo kwenye majukum mengine ya kikazi na kukabidhi misaada mbalimbali ikiwemo Mbuzi mmoja, Mchele, Sukari, Mafuta ya kupikia, Chumvi, Vinywaji, Maharage pamoja na Sabuni za kufulia na kuogea
Wanafunzi na mkurgenzi wao bi Aines Samweli wakifurahia zawadi zilizotolewa kwa ajili ya sikukuu
Picha na Thomas Ntobi-Afisa habari wa halmashauri ya wilaya ya Karagwe