Karagwe FM

(KDU) LTD Kukusanya zaidi ya Sh. Mil 86 kwa Mwaka 2024

19 December 2023, 8:32 pm

Karagwe

Na David Geofrey

Kayanga Duka la Ushirika (KDU) L.T.D inakusuduia kukusanya zaidi ya shilingi milioni 86 kutoka katika  vyanzo mbalimbali vya mapato kwa mwaka 2024 na kuendeleza miradi yao.

Akiwasilisha taarifa ya utekelezaji mbele ya wajumbe wa mkutano mkuu wa Kayanga duka la Ushirika (KDU LTD) Dec 19 mwaka huu,Bwana Robert Japhet Runyoro ambaye ndiye mwenyekiti, amesema pesa hizo Milioni 86,008,244.27/= zitakusanywa kutoka katika kodi zitokanazo na majengo wanayoyamiliki,viingilio pamoja na miradi mingine waliyo nayo.

Ili kutekeleza sheria za Ushirika, Bwana Josephat Kahungya Funga aliyeongoza kikao hicho baada ya kuchaguliwa kama mwenyekiti wa mkutano mkuu wa mwaka huu amesema ameridhishwa na bodi inayoongoza ushirika huo na kwamba mikakati iliyowekwa itatekelezwa ikiwa ushirikiano utapewa kipaumbele.

Bwana Wallace Mashanda mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya Karagwe ambaye ndiye aliyekuwa Mgeni rasmi katika mkutano huo amewapongeza wanaushirika huo kwakuendeleza na kulinda miradi iliyoanzishwa na waasisi wa ushirika huo na kuahidi kutoa ushirikiano utakapohitajika kwaajili ya kutekeleza shughuli mbalimbali za kimaendeleo.