Askofu Dkt. Bagonza atoa ujumbe mzito kwa wachungaji wapya
10 December 2023, 10:27 pm
Na Eliud Henry
Askofu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Karagwe Mchungaji Dkt. Benson Kalikawe Bagonza amewataka wachungaji waliobarikiwa kutofanya maamuzi wakiwa na Hasira na kuwasisitiza kusikia kile ambacho wengine hawawezi kusikia.
Amesema hayo Desemba 10 mwaka huu katika Ibada ya Kutabaruku Kanisa Kuu la Dayosisi ya Karagwe lililopo katika usharika wa Lukajange kata ya Bugene iliyoambatana na ubarikio wa wachungaji watano katika Dayosisi hiyo na kufanya Idadi ya wachungaji walio hai 105 katika Dayosisi hiyo.
Aidha, wachungaji waliobarikiwa wakapata nafasi ya kusema neno la Shukrani.
Kwa upande wake mgeni rasmi katika tendo hilo la Baraka Naibu Waziri Mkuu na waziri wa nishati Dk. Dotto Biteko aliyemwakilisha rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameishukuru Dayosisi ya Karagwe kipekee kwa kumpa nafasi ya kushiriki zoezi la Kutabaruku kanisa.
Hata hivyo, tendo hili la Kutabaruku kanisa limehudhuriwa na Baba Maaskofu wa KKKT, Roman Catholic na viongozi wa kitaifa akiwemo Makamu Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi CCM Tanzania bara Bw. Abdulrahman Kinana, Waziri wa Ujenzi Bw. Innocent Bashungwa pamoja na viongozi wa mkoa na wilaya.