Karagwe FM

TUWAKA Saccos kukusanya zaidi TSh. mil. 507 mwaka 2024

2 December 2023, 10:58 pm

TUWAKA SACCOS LTD (Tufaane Walimu Karagwe na Kyerwa) ni ushirika wa akiba na mikopo unaojengwa na walimu wote wa Karagwe na Kyerwa pamoja na wafanyakazi walioko chini ya Mkurugenzi wa Halmashauri

Wanacha wa TUWAKA SACCOS LTD waliohudhuria Mkutano mkuu wa 18 mwaka 2023

Na Ospicia Didace

Kyerwa

Mrajisi msaidizi wa vyama vya ushirika mkoa wa Kagera amekipongeza chama cha Akiba na Mikopo Karagwe na Kyerwa TUWAKA SACCOS Ltd kwa kuendelea kupata faida kubwa na kujitosheleza kwa fedha za  mikopo bila kuwa na madeni.

Amesema hayo mgeni rasimi na  mrajisi msaidizi wa vyama vya ushirika mkoa wa Kagera Robart George katika mkutano mkuu wa 18 wa Mwaka 2023 wa TUWAKA SACCOS Ltd uliofanyika katika ukumbi wa Rwelu Plaza wilayani Kyerwa Disemba mosi 2023

Sauti ya Mrajisi msaidizi wa vyama vya ushirika mkoa wa Kagera Bw. Robart George
Mrajisi msaidizi wa vyama vya ushirika mkoa wa Kagera Bw. Robart George

George Ameeleza kufurahishwa na taarifa ya mkaguzi wa nje aliesema kuwa chama hicho mpaka sasa kina faida zaidi huku akiwaomba wananchama kuongeza akiba zao ili kutunisha mkopo na kuepuka chama kwenda kukopa kwenye taasisi nyingine za fedha.

Sauti ya Mrajisi msaidizi wa vyama vya ushirika mkoa wa Kagera Bw. Robart George

Pamoja na hayo amewataka wanachama wa Tuwaka kutokupunguza akiba zao na kuweka kipaumbele katika maisha yao huku wakiepuka maisha ya kuiga.

meneja wa TUWAKA SACCOS Ltd Rogatus Rweikiza

Kwa upande wake meneja wa TUWAKA SACCOS Ltd Rogatus Rweikiza akisoma Risala mbele ya mgeni rasimi amesema kuwa pamoja na mafanikio yaliyopo kwenye SACCOS hiyo bado wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo baadhi ya wanachama kutokuwa na sifa za kukopesheka kutokana na kuwa na mikopo sehemu nyingine

Sauti ya Meneja wa TUWAKA SACCOS Ltd Rogatus Rweikiza

Mkutano huo umeambatana na uchaguzi  wa wajumbe wa bodi ikiongozwa na mwentekiti Bw Leonart Bechumila ,kamati ya usimamizi ,kamati ya huduma za jamii na mwakilishi mjumbe nje ya bodi.

Hata hivyo chama cha TUWAKA SACCOS Ltd kwa mwaka 2024 kinakisia kukusanya zaidi ya shilingi milioni  507 kutoka vyanzo mbali mbali vya mapato ikiwemo Riba za wanachama.