KKKT Dayosisi ya Karagwe inashirikiana vyema na Serikali Kutoa huduma za kijamii
30 October 2023, 9:11 pm
Zaidi ya shilingi milion 27 zimekusanywa katika harambee ya ujenzi wa kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania Dayosisi ya Karagwe, mtaa wa Nyabwegira usharika wa Nyabwegira uliopo katika Jimbo la Lukajange.
Na Jovinus Ezekiel
Karagwe
Serikali wilayani Karagwe imepongeza jitihada zinazoendelea kutekelezwa na kanisa la kiinjiri la Kilutheri Tanzania Dayosisi ya Karagwe katika utoaji wa huduma katika sekta ya afya na elimu wiayani Karagwe.
Akizungumuza katika harambee ya kuchangia mradi wa ujenzi wa kanisa la mtaa wa Nyabwegira usharika wa Nyabweigira jimbo la Lukajange dayosisi ya karagwe iliyofanyika katika mtaa huo octoba 29, 2023 mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Karagwe Walles Mashanda aliyemwakilisha mbunge wa jimbo la Karagwe ambaye pia ni waziri wa ujenzi Innocent Bashungwa amesema kuwa kanisa la kiinjiri la kilutheri Tanzania dayosisi ya karagwe limekuwa likifaya kazi kubwa ya kushirikiana na serikali katika utoaji wa huduma mbalimbali za kijamii wilayani Karagwe.
Amesema kuwa miongoni mwa huduma hizo ni utoaji wa huduma ya sekta ya afya hususani uwepo wa hosipitali ya Nyakahanga, na sekta ya elimu kwa kuanzisha taasisi za vyuo na shule za msingi na sekondari.
Awali akiwasilisha taarifa ya hali ya mradi wa ujenzi wa kanisa la mtaa wa Nyabweigila kwa mgeni rasmi katibu wa ujenzi wa mtaa huo Denice Migani amesema kuwa wazo la waumini kuanza mradi wa ujenzi wa kanisa lilianza mwaka 2010 kutokana na idadi ya waumini kuongezeka na mwaka 2023 mwezi januari walianza jitihada za ujenzi wa mradi huo ambao matarajio ili uweze kukamilika utagharimu milioni 200 na mpaka sasa zimeshatumika zaidi ya milioni 84 hadi hatua ya upauaji na kwa sasa zinahitajika zaidi ya milioni 62 ili ukamilike.
Aidha katika harambee hiyo ambayo imeendeshwa na mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya Karagwe Walles Mashanda zaidi ya milioni 27 zimepatikana ikiwemo fedha tasilimu na ahadi kutoka kwa wadau mbalimbali wa kanisa hilo ambapo mbunge wa jimbo la Karagwe na Innocent Bashungwa miongoni mwa fedha hizo amechangia milioni tatu.
Hata hivyo Askofu wa kanisa la kiinjiri la Kilutheri Tanzania dayosisi ya karagwe mchungaji Askofu Dr Benson Bagonza ambaye ameweka jiwe la msingi katikajengo hilo amesema kuwa kwenye ujenzi huo atachangia mabati yote ya jengo hilo hadi kukamilika na kuwapongeza waumini walioshiriki arambee hiyo pamoja na wadau wa maendeleo kutoka madhehebu mbalimbali ya kikirsto na kiisilamu.