Karagwe FM

Jukwaa la Uwezeshaji wanawake Kiuchumi Tanzania laja na Fursa lukuki

20 September 2023, 6:59 pm

Mwenyekiti wa Jukwaa la wanawake  wilaya ya Karagwe Leah John amewataka wanawake kutumia fursa za makongamano mbalimbali ili kubadilishana maarifa na kuinuana kiuchumi bila kujali viwango vya vipato vyao.

Na. Ospicia Didace

Mwenyekiti wa Jukwaa la wanawake  wilaya ya Karagwe Leah John amewataka wanawake kutumia fursa za makongamano mbalimbali ili kubadilishana maarifa na kuinuana kiuchumi bila kujali viwango vya vipato vyao.

Akizungumza na wanawake katika kongamano la jukwaa la wanawake la kuwainua kiuchumi lililofanyika katika ukumbi wa Mjeruman Garden mjini Kayanga wilayani Karagwe sep 20, 2023.

Mwenyekiti wa Jukwaa la wanawake  wilaya ya Karagwe Leah John: Picha na Ospicia Didace

Bi. Leah  amesema wanawake wanapaswa kushirikiana na kupeana fursa mbalimbali pale zinapojitokeza na kutumia majukwaa ya uwezeshaji wanawake kiuchumi kujiinua na kuwainua wengine.

Sauti Mwenyekiti wa Jukwaa la wanawake  wilaya ya Karagwe Leah John

Akizungumza katika kongaano hilo kwa niaba ya mkuu wa wilaya Karagwe Kareem Amri ambaye ni mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM Taifa amesema ni muda wa wanawake kujiinua kiuchumi na kufikia mafanikio na kuahidi kusaidiana na mwenyekiti wa jukwaa hilo kuhakikisha wanawake wanapata ardhi kwa ajili ya kilimo.

Sauti ya mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM Taifa Ndg. Kareem Amri

Pamoja na hayo Kareem amesema kuwa dhamira ya Mhe. Rais ni kumuona kila mwanamke  amewezeshwa kiuchumi akisema kuwa hakuna muujiza wa kuinuka kiuchumi bila kufanya kazi hivyo akawataka wanawake hao kufanya kazi kwa bidii.

Bi. Goleth Elias ni Meneja wa Karagwe Women SACCOS (KAWOSA) ni mmoja kati ya waweshaji ambae ameeleza maana ya uchumi na kuwataka kuwa na mawazo mapana ili kujiinua kiuchumi na kuepuka kila kitu kuwategemea wanaume.

Sauti ya Bi. Goleth Elias

Pia Bi. Goleth amewaomba akina mama kujitokeza kwenye frusa mbalimbali za maendeleo na kueleza mwanamke aliefanikiwa anakuwa na uwezo mpana wa kuchanganua mambo katika familia yake na taifa kwa ujumla.

Baadhi ya wanawake waliohudhuria kongamano la jukwaa la wanawake wilayani Karagwe lilifanyika Septemba 20, 2023: Picha na Ospicia Didace