Karagwe FM

Wazee wanolewa kuhusu matumizi bora ya fedha

11 September 2023, 9:58 pm

Rais wa shirika la Shina Inc Bi. Jesca Kamala Mushala akikabidhi fedha kiasi cha sh. mil. 1.2 kwa mwenyekiti wa SACCOS ya Abalakimala: Picha na Eliud Henry

Wazee wa kikundi cha wazee Bikolweengozi kata ya Bugandika wilayani Missenyi wameanzisha chama cha kuweka akiba ya fedha na kukopa kwa lengo la kujiinua kiuchumi.

Na: Jovinus Ezekiel

Missenyi

Mwenyekiti wa kikundi cha wazee Bikolweengozi cha kata ya Bugandika wilayani Missenyi mkoani Kagera  Audax Rwegalurila amesema kuwa chama cha kuweka akiba na kukopa ambacho kimeshapata usajili kwa sasa kinatambulika kama Abalakimala Saccos ambayo wamelenga iwasaidie kujiinua kiuchumi.

Amesema kuwa kutokana na kiasi cha fedha kidogo kidogo  ambacho wanajiwekea kwenye saccos yao wamelenga iwasaidie kuanzisha miradi mbalimbali ikiwemo kuanzisha duka la kikundi , kupata bima ya afya pamoja na kukopeshana wakati mwanakikundi anapopata shida kwani hata uongozi wa shirika la shina Inc umewasaidia sana kuboresha sacoss hiyo.

Sauti ya Audax Rwegalurila mwenyekiti wa SACCOS

“fedha kidogo kidogo  tunayoiweka kwenye SACCOS itatusaidia kuanzisha miradi mbalimbali ikiwemo kuanzisha duka la kikundi , kupata bima ya afya pamoja na kukopeshana wakati mwanakikundi anapopata shida kwani hata uongozi wa shirika la shina Inc umetusaidia sana kuboresha sacoss yetu”

Rais wa shirika la shina Inc B, Jesca Kamala Mushala amesema kuwa kilichompa msukumo kwa kushirikiana na  mlezi wa shirika hilo Bw,Amos Mgisha Mushala ili kuanzisha wazo la wazee hao wa kata ya Bugandika kutoka vijiji saba ambavyo ni Igulugati, Bwoki,Katendangulo,Rukulungo, Kijumo, Butulage na Bwemela kupata kikundi cha wazee Bikolweengonzi ni kutokana na upendo wa  mama yake mzazi marehemu B, Yuliana Kokwitika  kwa wanawake wenzake ambapo baada ya kuzeeka alikuwa akipata watu wa kumutembelea suala ambalo kwa wazee wengine kwa sasa baada ya kuzeeka hukosa watu wa kuwatembelea na kuwapa faraja .

Sauti ya Jesca Kamala Mushala

Naye mlezi wa shirika la shina Inc Bw, Mushala amesema kuwa wao kama shirika wanajivunia kuona wazee wanaendelea kunufaika na kikundi chao.

Naye  Joanes Chamushala  mkurugenzi wa shirika la shina Tanzania ambalo liko chini ya shirika la shina Inc amepongeza uongozi wa shirika la shina Inc kwa kuendelea kusadia wazee wa kikundi hicho kupitia utaratibu wa kuwakutanisha kila jumamosi ya wiki katika kijiji cha Igulugati kwa kuwagharimia usafiri, chakula na kuwapa fursa ya kufanya mazoezi ya viungo

Sauti ya Joanes Chamushala  mkurugenzi wa shirika la shina Tanzania