Wazee watakiwa kuchangamkia bima ya afya
10 September 2023, 8:53 pm
Na. Jovinus Ezekiel
Missenyi
Wazee katika kata ya Bugandika wilayani Missenyi mkoani Kagera wametakiwa kujiunga na bima ya afya ya CHF iliyoboreshwa kwa lengo la kuwawezesha kunufaika na huduma za matibabu.
Akiongea na wazee wa kikundi cha wazee Bikolw’engonzi kilichopo katika kata ya Bugandika wilayani Missenyi ambacho kinafadhiliwa na shirika la shina Inc lenye makao makuu nchini marekani kwa kuwakutanisha wazee kwa pamoja ili kutatua baadhi ya changamoto zinazowakabili pamoja na kubadilishana mawazo.
Mganga mfawidhi wa zahanati ya Bugandika Jesto Kisambale amesema kuwa wazee hao pamoja na wazee wengine ambao hawako katika kikundi hicho katani humo inabidi wajiunge na huduma ya bima ya afya ya CHF iliyoboreshwa.
Amesema kuwa endapo wazee watajiunga na bima hiyo itawasadia kunufaika na huduma ya matibabu toafuati na ilivyo sasa ambapo baadhi yawazee hawana bima.
Naye Bi. Jesca Kamala Mushala rais wa shirika la shina Inc ambalo limejikita katika utoaji wa Huduma kwa makundi mbalimbali ya wazee, watoto,wanawake na vijana katika nyanja mbalimbali za kuwajengea uwezo kiuchumi na kutoa huduma ya elimu katika mikoa mbalimbali ya Tanzania bara na visiwani Zanzibar amesema kuwa lengo la shirika hilo ni kuhakikisha wazee wa kikundi cha wazee Bikolw’engonzi wanapata bima.
Hata hivyo nao baadhi ya wazee wa kikundi hicho Audax Mlokozi na Demetilia Pasikale wamesema kuwa suala la kupata bima ni muhimu kwao ili kunufaika na huduma za matibabu.