Fursa kibao za ajira zatangazwa kwaajili ya Wananchi
28 September 2022, 6:53 pm
Wananchi wilayani Karagwe wamehimizwa kujiandaa ili waweze kunufaika kiuchumi kupitia Ujio wa mbio za Mwenge wa Uhuru utakao kesha katika uwanja wa changarawe Kayanga October 08 mwaka huu.
Ni wito uliotolewa na mkuu wa wilaya Karagwe Mwalimu Julieth Binyura Sept 28 mwaka huu wakati alipozungumza na redio Karagwe fm sauti ya wananchi Ofisini kwake ambapo amesema ujio wa Mwenge wa uhuru mwaka huu, Ni neema kwani wananchi watainuka kiuchumi na kimaendeleo.
Mwalimu Binyura akaeleza shughuli nzima ya mapokezi ya mwenge huo, na kuwataka wananchi kujitokeza kwa wingi siku hiyo.
Mbio za mwenge mwaka 2022 zilizinduliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Isdor Mpango katika viwanja vya Saba saba, mkoani Njombe tarehe 2 Aprili 2022, Na kilele chake itakuwa Oktoba 14, 2022 hapa mkoani Kagera.