Makarani na Wasimamizi 409 wa Sensa Wapigwa msasa
2 August 2022, 3:08 pm
Jumla ya watu 409 waliopita kwenye usaili wa kusimamia zoezi la sensa ambao ni makarani,wasimamizi wa maudhui na TEHAMA wameanza kupigwa msasa kwa kupewa mafunzo juu ya ukusanyaji sahihi wa takwimu za watu na makazi wakati wa sensa itakayofanyika tarehe 23 Agosti 2022
Akiongea na waandishi wa habari Mratibu wa Sensa Wilaya Missenyi Joachim Joseph Nyanda amesema kuwa mafunzo kwa wasimamizi hao yameanza tarehe 31 Julai 2022 katika Ukumbi wa shule Kiingereza Bunazi Green Acres na kwamba yatadumu kwa siku 19 mpaka tarehe 18 Agosti 2022.
Bwana Nyanda amesema kuwa baada ya kukamilika mafunzo siku tatu za awali kabla ya siku ya sensa makarani watakwenda kujitambulisha kwa viongozi wa maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya kuhesabia watu na makazi ikiwa ni pamoja kujaza dodoso la jamii linalolenga kutambua huduma za kijamii zinazopatikana katika eneo husika na kusoma na kutambua ramani ya maeneo ya kuhesabia.
“Nawaomba viongozi na wananchi wote Missenyi toeni ushirikiano kwa makarani wa sensa kwa kutoa taarifa sahihi zinazohusu wanakaya watakaolala kwenye kaya usiku wa kuamkia siku ya sensa” Amesema Nyanda
Aidha amewahakikishia wananchi kwamba taarifa zote watakazotoa zitabaki kuwa siri na kwamba wasiwe na wasiwe na wasiwasi