CWT Kagera, jiungeni na Benki ya Walimu
16 December 2021, 3:22 pm
Katibu wa chama cha Walimu Tanzania CWT Mkoa Kagera Tinda Paulini amewaasa viongozi wa chama hicho wilayani Missenyi mkoani Kagera kuwekeza katika Benki ya Walimu ili kuondokana na mikopo kandamizi inayotolewa na baadhi ya taasisi za kifedha
Akifunga mafunzo kwa viongozi hao yaliyofanyika katika Ukumbi wa Nyabutaizi Park Desemba 14, 2021 Katibu wa CWT Mkoa Kagera Mwl Paulini amewataka Walimu kuwekeza kwenye benki yao
“Njia pekee ya kuondokana na mikopo kandamizi ni Walimu kuwekeza kwenye benki yetu kwakufungua akaunt nakupitisha mishahara yetu ili kukuza mtaji utakaotuwezesha kukopa kwa masharti tuliojiwekea sisi wenyewe” amesema Mwl Tinda
Kwa Upande wake Katibu wa CWT Missenyi Mwl Rosemery Mboneko amesema kuwa mwitikio wa viongozi wa Chama Cha Walimu kuwekeza katika Benki yao ni Mkubwa Wilayani Missenyi nakwamba zaidi ya asilimia 85 ya Viongozi walioshiriki kwenye mafunzo wameamua kufungua akaunt na wengine kupitisha mishahara kwenye Benki hiyo