Jeshi la Akiba laomba kupewa kipaumbele.
23 November 2021, 6:32 pm
Wahitimu wa Mafunzo ya awali ya Jeshi la akiba Wilaya Missenyi Mkoani Kagera wameiomba serikali kuwatafutia ajira kwa kuwapa kipaumbele katika nafasi za kazi ya Ulinzi zinazotangazwa serikalini na katika taasisi binafsi
Katika Risala ya wahitimu iliyosomwa na MG Renatus Rwekaza Gerald wakati wa sherehe yakuhitimu iliyofanyika Katika Kata Kilimilile tarehe 19 Novemba 2021wamemuomba Mgeni rasmi Mkuu wa Wilaya Missenyi Kanali Wilson Sakullo kuwapa kipaumbe katika nafasi za ajira ya Ulinzi
Aidha amesema kuwa wahitimu wanao weledi wakutosha katika masuala ya ulinzi na usalama kutokana na mafunzo waliyopata kwa kipindi cha miezi minne kwenye kozi ambapo ametaja baadhi ya mada walizojifunza kuwa ni pamoja na utimamu wa mwili,mbinu za kivita,ujanja wa porini,huduma ya kwanza,uwezo wakutumia silaha mbalimbali na kwata
Kaimu Mshauri wa mgambo Wilaya Missenyi Meja Hango amewaondolea hofu yakukosa ajira wahitimu kwakutaja maeneo yenye fursa ajira ya kazi ya Ulinzi katika Kampuni binafsi, Halmashauri za Wilaya,Migodini pia akawahidi kuwapa kipaumbe pindi fursa itakapojitokeza yakupata mafunzo kwenye Jeshi la kujenga Taifa JKT
Naye Mkuu wa Wilaya Missenyi Kanali Wilson Sakulo amewataka wahitimu kutumia vizuri mafunzo waliyopata kwa manufaa ya jamii, Wilaya Missenyi na Taifa kwa ujumla.