Sensa ya majaribio kufanyika Sept 11,2021
31 August 2021, 11:10 am
Wakazi wa Kijiji cha Mutukula kilichoko Missenyi Mkoani Kagera wametakiwa kutoa ushirikiano ili kufanikisha sensa ya majaribio itakayofanyika tarehe 11 Septemba 2021
Akihamasisha Wananchi kushiriki zoezi la majaribio ya sensa katika Mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Mutukula kilichoko Mpakani mwa nchi ya Tanzania na Uganda tarehe 28 Agosti 2021
Kamisaa wa Sensa na Spika Msitaafu Anna Semamba Makinda amesema kuwa Kijiji cha Mutukula ni miongoni mwa Vijiji 13 Tanzania bara itakapofanyika sensa ya majaribio ikiwa ni moja ya hatua za maandalizi ya Sensa ya watu na makazi itakayofanyika mwaka 2022
Amesema kuwa wakazi wa Kijiji hicho wahakikishe wanashiriki kikamilifu zoezi hilo linalolenga kutoa picha halisi sensa nakuwezesha waandaaji kupima nyenzo zitakazotumika wakati wa sensa na mfumo mzima wa utekelezaji wa mpango kazi wa Sensa
Amesema kuwa wakati wa sensa ya majaribio watu wote watakaolala ndani ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania watahesabiwa hivyo akawataka wananchi kutoa ushirikiano kwa Makarani kwakujibu Maswali yote watakayoulizwa kwa usahihi ili kujaza dodoso la sensa lenye taarifa muhimu kwa Maendeleo ya Taifa la Tanzania.
Awali akisoma taarifa ya maandalizi ya Sensa ya majaribio Mkuu wa Wilaya Missenyi Kanali Wilson Sakullo amesema kuwa tayari eneo ambapo watu watahesabiwa limeshatambuliwa na mafunzo kwa Waratibu na Makarani watakaoshiriki kwenye zoezi la sensa yanaendelea Mkoani Iringa
Sensa ya majaribio inafanyika katika Mikoa 18 iliyochaguliwa,Mikoa 13 ya Tanzania Bara katika Wilaya 13 na Mikoa 5 ya Zanzibar katika Wilaya 10
Tazama sehemu ya hotuba ya Kamisaa wa Sensa na Spika Msitaafu Anna Semamba Makinda akiongea na Wakazi wa Kijiji Cha Mutukula juu ya umuhimu Sensa kwa Maendeleo ya Taifa.