Agizo kwa waliopata Hati yenye mashaka.
29 June 2021, 8:22 am
Mkuu wa mkoa wa Kagera Meja General Charles Mbuge ameliagiza baraza la madiwani wa Halmashauri ya wilaya Karagwe mkoani Kagera kuhakikisha linawachulia hatua za kisheria watumishi waliobainika kutumia vibaya madaraka ya ofisi na kusababisha Halmashauri hiyo kupata hati ya mashaka kwa mwaka wa fedha 2019/2020.
Agizo hilo la Rc -Meja General Charse Mbuge limetolewa hivi karibuni kupitia kikao maalumu cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya wilaya ya Karagwe kilichoketi kujadili taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi wa Hesabu za serikali CAG, kwa mwaka wa fedha 2019/2020 ambapo Halmashauri ya wilaya Karagwe imepata Hati yenye mashaka.
Baadhi ya madiwani wa Halmashauri ya wilaya Karagwe akiwemo Evalistha Sylivester wa kata Kiruruma pamoja naye Justine Fidelis wa kata Nyakabanga wamesema halmashauri hiyo imepata hati yenye mashaka kutokana na uzembe uliofanywa na baadhi ya watumishi wa Halmashauri hiyo wakati wa ukusanyaji wa mapato ya ndani.