Karagwe FM
Shilingi milioni 626 kukarabati shule wilayani Karagwe
4 May 2021, 11:09 am
Halmashauri ya wilaya Karagwe imepokea shilingi milioni 626 kwa ajili ya ukarabati na ujenzi wa miundombinu katika baadhi ya shule za msingi na Sekondari wilayani Karagwe mkoani Kagera.
Taarifa hiyo imetolewa na mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Karagwe Wallace Mashanda ambae pia ni diwani wa kata ya Nyaishozi wakati akifungua mkutano wa baraza la madiwani lililoketi katika ukumbi wa angaza mjini Kayanga mwishoni mwa mwezi April 2021.
Mashanda amesema kuwa pesa iliyotolewa itachangia pakubwa katika kupunguza adha wanayoipata wanafunzi wanaotumia miundombnu mibovu katika shule za msingi na sekondari.
Mwandishi wetu Ospicia Didace anaripoti