Karagwe FM
Madereva walia na ubovu wa stendi.
28 April 2021, 1:49 pm
Madereva wa Tax katika stendi ya Kayanga wilaya ya Karagwe Mkoa Kagera wameiomba serikali wilayani humo kufanya marekebisho ya stendi kutokana na stendi hiyo kujaa maji na tope wakati wa masika.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya Karagwe bwana Wallece Mashanda amekiri kuwepo kwa changamoto hiyo na kwamba taratibu za kuikarabati zinaendelea hivyo amewaomba madereva tax kuwa wavumilvu.