Wakosa makazi kwasababu ya Mafuriko.
26 April 2021, 8:20 pm
Mvua zinazoendelea kunyesha katika sehemu mbalimbali Wilayani Missenyi zimesababisha baadhi ya barabara za mitaa na makazi ya watu katika mji mdogo wa Kyaka Bunazi kujaa maji huku baadhi ya wakazi wa mji huo wakilazimika kuhama makazi
Mkuu wa Wilaya Missenyi Kanali Denisi Mwilla na Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya Missenyi Innocent Mukandala,Meneja wa TARURA Missenyi wamekagua barabara zilizoharibika pamoja na Wananchi walioathirika ili kujionea ukubwa wa tatizo nakuchukua hatua stahiki zinazotakiwa kwa sasa.
Mkuu wa Wilaya Missenyi Kanali Denisi Mwilla amesema kuwa wamechukua hatua mbalimbali ambapo kuanzia usiku wakuamkia leo jumatatu wataalam kutoka wakala wa barabara za Vijijini na Mijini TARURA Missenyi wanashirikiana na wataalam kutoka kiwanda cha sukari Kagera Sugar wanafanya kazi yakuangalia jinsi yakuzibua mitaro iliyoziba ili Maji yatoke pia wametoa taarifa ngazi za juu serikalini kuomba misaada kwa waathirika.