Neema yawashukia wajasiriamali.
16 April 2021, 12:21 pm
Mji mdogo wa Kyaka Bunazi ulioko Wilayani Missenyi ni maarufu Mkoani Kagera kwa kuuza ndizi za kuchoma zinazoitwa gonja ambapo makumi ya wanawake na vijana wanafanya biashara hiyo ili kujipatia kipato kwa kuwauzia gonja abiria wanaosafiri na magari yanayopita katika Stendi hiyo wakitokea sehemu mbalimbali ndani na nje ya Nchi
Tarehe 16 April 2021 Kamati ya fedha Utawala na Mipango Halmashauri ya Missenyi imefanya ziara yakukagua Mradi wa Ujenzi wa jengo la wauza gonja ili kujiridhisha na thamani ya fedha kiasi cha shilingi milioni 50 walizopitisha kwa ajili ya Ujenzi wa jengo hilo.
Mwenyekiti wa kamati ya Ujenzi wa stendi Mosses Ngonya amesema kuwa Ujenzi wa jengo hilo umefikia asilimia 60 nakwamba licha yakutengewa milioni 50 wanakadiria kutumia shilingi milioni 40 nakwamba fedha zitakazobaki zitaboresha miundombinu mingine kama kuweka taa ili stendi ifanye kazi usiku na mchana.
Mmoja kati ya akina mama wanaofanya biashara ya gonja bi Martha Ayubu ameishukuru halmashauri kwakuwajengea jengo hilo kwamba litawasaidia kumaliza tatizo lakunyeshewa mvua wakati wakuchoma gonja na mengineyo yatakanayo nakuchomea gonja juani.Bi Martha pia ameiomba serikali kuwawezesha mikopo isiyo na riba ili waondokane na riba kubwa kutoka taasisi nyingine za kifedha wanakojikopesha ambapo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri Innocent Mukandala ameagiza Idara ya Maendeleo ya jamii ifike nakutoa Elimu ya mikopo kwa wafanyabiashara wanaouza gonja katika stendi hiyo
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya Missenyi Projestus Tegamaisho amesema kuwa Kamati imeridhika na hatua ya Ujenzi wa jengo hilo pia akawahakikishia wananchi kwamba wanaendelea kuboresha mazingira ya Stendi ya Kyaka ili iwe yakisasa kwakutenga fedha nakuwa mwaka ujao wa fedha wametenga milioni 47