Zenj FM

Wanahabari Pemba waaswa kuandika habari za kuinua sauti za wanawake 

6 November 2024, 5:15 pm

Mjumbe wa bodi ya Tamwa Zanzibar Mwatima Rashid Issa akizungumza na waandishi wa habari walipokuwa kwenye mafunzo ya mabadiliko ya tabia nchi yanayolenga kusaidia mwanamke kupaza sauti yake pamoja na uongozi. Picha na Is-haka

Na Is-haka Mohammed.

Waandishi wa Habari kisiwani Pemba wameaswa  juu kuandika Habari zitakazosaidia kuwezesha kusikiika kwa sauti za wanawake zinazohusu mabadiliko ya tabia ya nchi  na athari zake, ili sauti za wanawake hao zipate kusikika na kuondokana na changamoto zinazojitokeza  za kupata haki zao za kutosikika.

Mjumbe wa Bodi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tamwa-Zanzibar Mwatima Rashid Issa ameyasema hayo wakati akizungumza na waandishi wanaoshiriki katika mafunzo  maalum ya yanayohusiana na mabadilo ya tabia nchi na athari zake hasa kwa wanawake na watoto yaliyofanyika  katika ukumbi wa ofisi  ndogo  za Tamwa zilizopo Mkanjuni Chake Chake.

Amesema Tamwa Zanzibar imebaini kuwepo kwa changamoto kubwa kwa waandishi wa habari kisiwani Pemba  katika kupaza sauti za wanawake wanaokabiliwa na changamoto za mabadiliko ya tabia ya nchi  jambo ambalo hurejesha nyuma wanawake hao  katika harakati zao.

Sauti ya Mjumbe wa Bodi wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tamwa-Zanzibar Mwatima Rashid Issa.

Akiwasilisha mada kwa waandishi wa habari Mwandishi wa  Mwandamizi anayeongoza mafunzo hayo ya Zan-Adapt, Ali Mbraouk Omar  amesema  shughuli  za kiasili  zinazofanywa na  binaadmu ikiwemo kukata miti, uvuvi haramu,  kuongezeka joto  na nyenginezo hupelekea kuleta athari   kwa akina mama na wanawake katika shughuli zao.

Sauti ya Ali Mbraouk Omar.

Awali akielezea mradi huo Afisa mawasiliano wa Tamwa Zanzibar Nafda Hindi Moh`d amesema kuwa lengo la mradi huo ni kuona waandishi wa habari visiwani hapa wanaandika habari zinazomnyanyua mwanamke katika kukabiliana na athari za mabadiliko ya tabia nchi na katika uongozi.

Sauti ya Afisa mawasiliano wa Tamwa Zanzibar Nafda Hindi Moh`d.

Nao baadhi ya waandishi wa Habari akiwemo Habiba Zarali  Rukuni  na Abdi Juma Suleiman wamesema mafunzo hayo yatawasaidia kubadilisha mitazamo yao katika kuandika Habari zinazowahusu  wanawake na mabadiliko ya tabia ya nchi.

Sauti za washiriki.

Mafunzo hayo ya siku 2  yanayotolewa  kwa waandishi wa habari 30,ikiwa 20 ni kutoka Kisiwani Unguja na 10 Pemba  ni utekelezaji wa mradi wa Zanz- Adopt unaotekelezwa  kwa mashirikiano kati ya Tamwa, Community Forest Pemba na Community forest International  kwa ufadhili wa  Canada.