Zenj FM

JUMAZA yahimiza malezi ya dini kwa vijana

23/03/2026, 14:56

Amiri wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar(JUMAZA) Shekh Farid Hadi Ahmed akizungumza na waumini wa dini ya kiislam katika mahafali ya sherehe za Eid Fitri huko katika msikiti wa Chachani Chake Chake.

Waumini wa dini ya Kiislamu wamehimizwa kuwalea vijana katika misingi ya maadili mema ili waweze kuijua vyema dini ya Allah. Wito huo umetolewa na Sheikh Farid Hadi Ahmed wakati wa mahafali ya Eid yaliyofanyika Chake Chake, Pemba.

Na Is-haka Mohammed

Waumini wa dini ya kiislam wameendelea kusisitizwa juu ya umuhimu wa  kuwapea vijana wao katika  misingi ya maadili mema yatakayo pelekea kuijua dini ya Allah S.W.

Wito huo umetolewa na Amiri wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar(JUMAZA) Shekh Farid Hadi Ahmed wakati akizungumza na waislamu katika mahafali ya Eid Al- Fitting aliondaliwa na Jumuiya hiyo Wilaya ya Chake Chake huko katika msikiti wa Chachani.

Amiri Farid amesema  wapo baadhi ya waislamu ambayo  hawawasimamii vizuri watoto wao katika kutenda mambo ya kheir ya kumcha Mwenyezi Mungu jambo linaweza kuwatumbukiza vijana hao kuangukia kwenye upotevu

Sauti ya Amiri wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar(JUMAZA) Shekh Farid Hadi Ahmed.

Akisoma Risala ya pamoja ya JUMAZA na Jumuiya ya Kuendeleza Elimu, Malezi na Maalidi kwa waislamu Pemba Naibu Amiri wa JUMAZA Shekh Omar Ali Salim amesema bado Jumuiya hiyo inaendelea na mchakato wa kutafuta wafadhili kwa ajili ya ujenzi ya hospitali ya kisasa ya waislamu.

Sauti ya Naibu Amiri wa JUMAZA Shekh Omar Ali Salim.

Mapema akitoa maelezo ya Qur-an ya ufunguzi wa mahafali hayo iliyosomwa na Shekh Khamis Ali Khamis, Mwenyekiti wa Istiqama for Development Wilaya ya Chake Chake Sheikh Mohammed Suleiman Al-tiwany amehimiza kuendeleza Umoja na mshikamano wa waislamu ili kuzishinda hila za maadui wa uislamu.

Sauti ya Mwenyekiti wa Istiqama for Development Wilaya ya Chake Chake Sheikh Mohammed Suleiman Al-tiwany.

Mahafali hayo hufanyika kila mwaka katika skukuu za idd Fitri na idd adhha na ujumbe wa mwaka huu ni umoja wetu ndio ushindi wetu.