Zenj FM
Zenj FM
19/02/2026, 16:56

Mahakama Kuu ya Zanzibar imetupilia mbali maombi ya kupinga matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar yaliyohusu wajumbe wa Baraza la Wawakilishi katika majimbo nane (8) ya Kiwani, Mkoani, Chake Chake, Chonga, Wawi, Wingwi, Micheweni na Kojani.
Na Mwandishi wetu.
Maombi hayo yalifunguliwa na baadhi ya waliokuwa wagombea wa nafasi ya Ujumbe wa Baraza la Wawakilishi kutoka Chama Cha ACT- Wazalendo wakipinga matokeo ya uchaguzi katika majimbo husika.
Katika uamuzi wake, Mahakama Kuu ya Zanzibar ilikubaliana na pingamizi zilizowekwa na upande wa walalamikiwa ambao ni Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar pamoja na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, kwamba maombi hayo yalikuwa na kasoro nyingi za kisheria.
Mahakama ilijiridhisha kuwa hati za kiapo (affidavits) zilizoambatanishwa na maombi hayo zilikuwa na kasoro za kisheria, na hivyo haziwezi kutambuliwa wala kuwa sehemu ya maombi yaliyowasilishwa mahakamani.
Kutokana na kasoro hizo, Mahakama iliamua kuyatupilia mbali maombi hayo.
Uamuzi huo umetolewa na Jaji Haji Khamis Suleiman