Zenj FM

Jamii ya Mikumi yainuka kiuchumi kupitia ushirikiano na TANAPA

3 December 2025, 5:28 pm

Mwenyekiti wa kikundi cha Tupendane Chekeleni COCOBA Vitalia Michpe, Kipanga.

Na Mary Julius.

Shirika la Hifadhi za Taifa Tanzania TANAPA  limeendelea kushirikiana kwa karibu na jamii inayozunguka Hifadhi ya Mikumi kwa lengo la kuimarisha uhifadhi na kuinua maendeleo ya wananchi.

Afisa Uhifadhi Daraja la Kwanza, Emakulata Mbawi, anayesimamia kitengo cha mahusiano ya jamii katika hifadhi hiyo, ameyasema hayo wakati wa ziara ya waandishi wa habari na wadau wa utalii kutoka Zanzibar waliotembelea kikundi cha Tupendane Chekeleni COCOBA kilichopo Mikumi, mkoani Morogoro.

Mbawi amesema TANAPA imekuwa ikiwasaidia wananchi kupitia vikundi vya Community Conservation Banks maarufu kama COCOBA, ambavyo vimekuwa chachu ya maendeleo na uhifadhi.

Kwa mujibu wa Mbawi, jumla ya vikundi 86 vilivyopo katika vijiji 8vimenufaika moja kwa moja na fedha mbegu zilizotolewa na TANAPA, huku vikundi vyote vikipewa elimu ya uhifadhi na utalii.

Sauti ya Afisa Uhifadhi Daraja la Kwanza, Emakulata Mbawi.

Katika ziara hiyo, Katibu Msaidizi wa kikundi cha Tupendane Chekeleni, Redi Daniel, amesema baada ya mafunzo walipatiwa fedha mbegu zaidi ya ambazo ziliwasaidia kukopeshana na kukuza mitaji ya mtu mmoja mmoja..

Sauti ya Katibu Msaidizi wa kikundi cha Tupendane Chekeleni, Redi Daniel,

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa kikundi hicho, Vitalia Michpe, Kipanga amesema kupitia COCOBA wamekuwa wakielimisha jamii juu ya madhara ya ukataji miti, matumizi ya mkaa, na ujangili, sambamba na kuhamasisha vijana kushiriki katika uhifadhi wa mazingira.

Sauti ya Mwenyekiti wa kikundi hicho, Vitalia Michpe, Kipanga.

 Nao Wanachama wa kikundi hicho wamesema kabla ya mradi maisha yao yalikuwa magumu, lakini sasa wameweza kujiinua kiuchumi na kuboresha maisha ya familia zao.

Sauti ya wanachama.

Kauli mbiu ya vikundi hivyo ni kufundisha wengine uhifadhi na utalii.