Zenj FM
Zenj FM
13 November 2025, 8:51 pm

“Mawaziri na manaibu waziri nilioteua hakikisheni mnatekeleza majukumu yanu kwa uwajibikaji, uadilifu na kasi ya maendeleo, ili kutimiza matarajio ya wananchi wa Zanzibar”
Na Mary Julius.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ametangaza Baraza jipya la Mawaziri wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Akizungumza Ikulu Mnazi Mmoja Zanzibar, Dkt. Mwinyi ametaja majina ya Mawaziri kumi na sita kati ya wizara ishirini, huku akibainisha kuwa wizara nne zimeachwa wazi kwa ajili ya Chama cha ACT Wazalendo, endapo chama hicho kitakubali kushiriki katika kuunda Serikali ya Umoja wa Kitaifa.
Dkt. Mwinyi amesema kuwa uamuzi wa kuacha nafasi hizo ni kwa mujibu wa sheria za Zanzibar, ambazo zinatoa muda wa siku tisini (90) kujaza nafasi hizo ndani ya Serikali.
Aidha, Rais Mwinyi amewataka mawaziri na manaibu waziri walioteuliwa kuhakikisha kuwa wanatekeleza majukumu yao kwa uwajibikaji, uadilifu na kasi ya maendeleo, ili kutimiza matarajio ya wananchi wa Zanzibar.