Zenj FM
Zenj FM
17 October 2025, 6:26 pm

Na Berema Suleiman Nassor.
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Vijana Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Zanzibar Shaibu Ibrahim Mohammed amewataka vijana kuwa mstari wa mbele katika kudumisha amani na utulivu wakati wa uchaguzi na baada ya uchaguzi.
Akizungumza katika mdahalo wa uchaguzi bila ya vurugu ulioandaliwa na taasisi ya Pamoja Youth Initiative amesema mdahalo huo si mkutano tu bali ni juhudi za kutunza Amani Zanzibar na Tanzania kwa ujumla kupitia uelewa na ushirikiano katika kuhakikisha uchaguzi wa mwaka 2025 unakuwa wa Amani umoja na ukomavu wa kidemokrasia.
Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa tasisi ya Pamoja Youth Initiative Rashid Mwinyi amesema malengo ya mdahalo huo ni kuimarisha ushirikiano kati ya tasisi za uchaguzi vyombo vya ulinzi na usalama mitandao ya vijana na mashirika ya kiraia ili kukuza ushiriki wa Amani na utulivu katika kipindi cha uchaguzi na baada ya uchaguzi.
Nae mkuu wa kurugenzi ya huduma za uchaguzi Khamis Issa Khamis amesema Tume ya Uchaguzi Zanzibar itaendelea kushirikiana na asasi mbalimbali za kiraia kwa lengo la kutoa elimu ya mpiga kura katika jamii sambamba na kudumisha Amani na utulivu nchini.
Mdahalo huo n ni hatua muhimu kuelekea kuimarisha misingi ya demokrasia Zanzibar kupitia Amani ushirikishwaji na uwajibikaji wa pamoja.