Zenj FM
Zenj FM
6 October 2025, 10:28 pm

Na Ivan Mapunda
“Niligombania mwaka 2020 katika nafasi ya uwakilishi jimbo la mfenesini ila kura zangu hazikutosha kura Nilipata kura 1 katika kura 100”
Katika uchaguzi wa uwakilishi uliofanyika katika jimbo la Mfenesini jina la Asha Juma Kombo lipo katika historia na lilibaki katika midomo ya watu wengi ,licha ya kupata kura 1 na kupitwa kwa kura 73 na mpinzani wake Machano Othuman Said safari yake ya kisiasa imeibua msisimko mpya kuhusu nafasi ya mwanamke katika uongozi.
Kwa wengine ,matokeo haya ingekua sababu ya ya kuvunjika moyo ila kwangu ilikua kama chachu na kunipa ujasiri ,lakini kwa asha ni toufauti kwake ni ushindi mkubwa na heshima iliyompa uthubutu na matumaini makubwa na kugombania ubunge katika jimbo la mfenesi na huu ni uthibitisho mkubwa kuwa wanawake wana uwezo mkubwa wakuongoza jamii kama watapewa nafasi .
Safari Ya Maisha Na Elimu
Katika medani ya siasa za Zanzibar, Asha Juma Kombo ni jina jipya linaloibuka kama alama ya uthubutu na uongozi jumuishi.
Asha juma kombo alizaliwa mwaka 1976 katika kijiji cha kicheche mkokotoni , wilaya ya kaskazini a, mkoa wa kaskazini unguja. Kwa sasa ana umri wa miaka 45 ni mama wa watoto 4 na mke wa Hussein Kassim Makame .
Elimu yake ya awali alipata katika skuli ya msingi potoa na baadaye akajiunga na skuli ya mkokotoni baada ya kufaulu michepuo mwaka 1996.
Aliendelea na masomo mpaka kufika shahada ya uzamivu katika fani ya elimu ya sanaa(master’s) katika chuo cha International Christian University (ICU)nchini Japani mwaka 2017 hatua kubwa inayoonyesha dhamira yake ya dhati kuleta mabadiliko ya kweli katika jamii.
Uzoefu Na Uwanachama Wa Kisiasa.
Asha ni mwanachama wa Chama Cha Mapinduzi (CCM ) tangu akiwa kijana alihudumu katika shehia ya mchangani kama mwanaharakati na mpenda mabadiliko ,uzoefu aliupata ukamjengea ujasiri wa kugombania kwa mara ya kwanza uwakilishi,akiwa na maono na mkakati wa kuisaidia jamii yake.
Cheo Chake Katika Serikali.
Cheo chake kwa sasa katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni mfanyakazi katika taasisi ya elimu .
Kazi yake ni kukuza mitaala ya elimu na kuboresha elimu kutoka maandalizi hadi chuo (collage )
Mwanzoni alikua mwalimu wakati anaanza kazi mwaka 2003 katika shule ya mtoni kigomeni .
vile vile alikua ni Katibu wa Baraza la Redempt katika kipindi cha mpasuko wa siasa shehia ya mchangani .
Sababu Za Kugombea.
Kilichonisukuma kugombania ni mapenzi ya dhati naya kweli ya jimbo la Mfenesini ,eneo ninalolifahamu kwa undani zaidi ni ameona ni wakati muafaka wa kuawa sauti ya watu,hasa wanawake,watoto na vijana na kuibua changamoto zinazowakabili.
“Napenda kuona nimesimamia changamoto za jamii mpaka zimetatuka kwangu mimi ni kama sadaka ”
Pia amelenga kuwajengea uwezo wanawake kwa kuwapa mafunzo ya uongozi elimu ya urai,siasa ili kuwatoa hofu na kukuza idadi ya wanawake.
Nimepanga kukuza kiwango cha michezo kwa watoto na vijana katika jimbo la mfenesini kwa kukuanzisha Sport Academy.
Changamoto na mafanikio
Changamoto kubwa niliyokutana nayo ni kubezwa kutokana na jinsia yake.
Wengi walinibeza kwa sababu mimi ni mwanamke lakini sikuvunjika moyo .
”Niliamini katika uwezo wangu na nilisimama kidete kugombania” …amesema kwa msisitizo Asha
Lakini ndani ya changamoto hiyo,alipata mafanikio makubwa mwanamke huyu alipambania kutatua changamoto ya maji kuingi katika nyumba zetu na kupelekwa bahari katika shehia ya mfenesini na kama kuptia progam ya sema na rais.
Aidha Mumewe Hussein Kassim Makame amekuwa nguzo muhimu katika maisha na safari ya kisiasa ya Asha . Akizungumzia mchango wa mke wake, alisema“Mke wangu ni mwanamke shupavu,Kila wakati amesimama kwa ajili ya familia na jamii na mimi nitabaki kumpa ushirikiano hadi atakapofanikisha malengo yake”.
Wito wangu ni wanaume wasimame bega kwa bega na wake zao wanapojitosa kwenye nafasi za uongozi.
Ushauri Kwa Wanawake
Wanawake wanatakiwa kujiamini ,kila kitu kinawezekana kama utajitolea na kuweka jitihada .uongozi ni haki ya kila moja wetu.
Pia anahimiza wanawake kusimama wenyewe na kutokubali kudhalilishwa na kutumika kama daraja kwa wengine.
“Hakuna mafanikio yanayopatikana kupitia mgongo wa mtu mwengine” anasema
Naamini siasa na mapenzi havichangamani bali ni uwito kutoka ndani ya nafsi , ili mwanamke afanikiwe lazima ajitambue,ajiheshumu ,ajue thamani yake na asimame kwa miguu yake.