Zenj FM
Zenj FM
6 October 2025, 5:51 pm

Na Is-haka Mohammed.
Mgombea Urais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha United Democratic Party(UDP) Saumu Hussein Rashid amewahidi wafanyabiashara na wajasirimali wadogo wadogo katika soko la Tibirinzi Chake Chake kuweka mazingira bora ya biashara ili awape kufanya shughuli zao kwa wepesi.
Mgombea huyo ametoa ahadi hiyo wakati alipotembelea soko hilo kwa lengo la kuangalia mazingira ya soko hilo la kuwasikiliza wafanyabiashara hao akiwa katika ziara yake kisiwani Pemba kwa ajili ya kufanya kampeni za kuomba kura za kuchaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Amesema lengo na azma ya Chama cha UDP ni kufungua fursa za kiuchumi ili kila mtanzania awe na uwezo wa kiuchumi na kupata kipato cha kujitosheleza na kukuza uchumi wa Taifa kwa ujumla.
Wafanyabiashara wa soko la Tibirinzi wamemweleza Mgombea huyo wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania changamoto ya utozwaji wa kodi kubwa jambo ambalo ninakwanza maendeleo ya biashara zao.
Mapema Mgombea huyo mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege wa Pemba alifika katika kijiji cha Wawi na kuzuru kaburi na aliyekuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Marehemu Dkt. Omar Ali Juma na kumtakia dua.