Zenj FM

Maendeleo kwa vitendo, Asha Juma aahidi mabadiliko mfenesini

27 September 2025, 10:10 pm

Spika wa Baraza la Wawakilishi, ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Zuberi Ali Maulid, akimnadi Mgombea wa Ubunge wa Jimbo la Mfenesini kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Asha Juma Kombo.

Na Ivan Mapunda.

Mgombea wa Ubunge wa Jimbo la Mfenesini kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Asha Juma Kombo, amesema endapo atapewa ridhaa ya kuwa mbunge, atahakikisha anakuza vipaji vya watoto na vijana kupitia ujenzi wa Sports Academy maalum katika jimbo hilo.

Akizungumza katika uzinduzi wa kampeni za uchaguzi uliofanyika kwa kishindo wilayani Mfenesini, Asha Juma Kombo ameeleza kuwa tayari amefanya mazungumzo na moja ya sports academy kubwa nchini Tanzania ambayo ina ushirikiano na nchi tano, ikiwa na lengo kuu la kukuza vipaji vya watoto na vijana kuanzia umri wa miaka 9.

Sauti ya Mgombea wa Ubunge wa Jimbo la Mfenesini kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Asha Juma Kombo.

Katika sekta ya elimu, Asha Juma Kombo ameahidi kushirikiana na walimu pamoja na wazazi ili kuongeza ufaulu wa wanafunzinakupunguza utoro mashuleni, akisisitiza kuwa elimu ni msingi wa maendeleo ya jamii.

Sauti ya Mgombea wa Ubunge wa Jimbo la Mfenesini kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), Asha Juma Kombo.

Nae Mgombea wa Uwakilishi wa Jimbo la Mfenesini, Machano Othman Said, amesema kuwa Chama Cha Mapinduzi kimefanikiwa kutekeleza kwa mafanikio makubwa ilani ya mwaka 2020-2025.

Aidha Ametoa wito kwa wananchi kujitokeza kwa wingi tarehe 29 Oktoba kwenda kukipigia kura CCM ili kiendelee kuleta maendeleo katika jimbo hilo.

Sauti ya Mgombea wa Uwakilishi wa Jimbo la Mfenesini, Machano Othman Said,

Katika hafla hiyo ya uzinduzi wa kampeni, viongozi mbalimbali wa CCM walihudhuria wakiwemo viongozi wa ngazi ya taifa, mkoa, wilaya pamoja na wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi.

Sauti za Viongozi.

Spika wa Baraza la Wawakilishi, ambaye pia niMjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Zuberi Ali Maulid, ndiye aliyefungua rasmi kampeni hizo.

Aidha  Ametoa wito kwa wananchi na wanachama wa CCM kujitokeza kwa wingi kupiga kura ili chama hicho kipate ushindi wa kishindo katika uchaguzi huo ujao.