Zenj FM

Wizara ya Afya na Maisha Meds watoa miwani bure kwa wenye Umri 40+

23 September 2025, 7:47 pm

Baadhi ya wananchi wakipatiwa huduma katika viwanja vya Mnazi mmoja Zanzibar.

Na Mary Julius.

Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Taasisi ya Maisha Meds imeanzisha zoezi la utoaji wa miwani kwa wananchi wenye umri wa miaka 40 na kuendelea, hasa wale wenye changamoto ya kuona vitu vya karibu.
Zoezi hilo linalofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja, ambapo Juma Bashir Juma kutoka taasisi ya Maisha Medis amesema huduma hiyo inalenga kusaidia jamii ya Wazanzibari, hususan wale wenye matatizo ya macho ambao hawawezi kuona vizuri vitu vya karibu .
Amehimiza wananchi wenye changamoto hizo kujitokeza kwa wingi ili kunufaika na huduma hiyo kabla haijakamalizika.
Kwa mujibu wa Juma, hadi sasa jumla ya vituo 24 vinatoa huduma hiyo ya miwani kwa sh 3000, na baada ya kipindi cha siku tano za zoezi la bure kumalizika, huduma hizo zitaanza kutolewa kwa malipo katika vituo hivyo.

Sauti ya Juma Bashir Juma.

Nao Wananchi waliopokea miwani kupitia mpango huu wameishukuru serikali na waandaaji wa programu kwa kuwasogezea huduma hiyo muhimu.
Aidha, wameishauri jamii kujitokeza kwa wingi kunufaika na fursa kama hizi zinazotolewa kwa lengo la kuboresha afya na ustawi wa wananchi.

Sauti ya wananchi.