Zenj FM
Zenj FM
11 September 2025, 8:11 pm

Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Jaji George Joseph Kazi ,amesema Tume hiyo imewateua rasmi wagombea kumi na mmoja (11) wanaowania nafasi ya Rais wa Zanzibar katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 na kuwakabidhi vyeti vyao vya uteuzi katika hafla iliyofanyika katika ofisi za Tume, Maisara Zanzibar.
Katika kuhakikisha kampeni zinafanyika kwa mazingira ya usawa, haki na amani, Tume ya Uchaguzi imekabidhi magari mapya aina ya land cruiser VXR kwa kila mgombea, pamoja na madereva na walinzi .
Wagombea walioteuliwa ni Dk. Hussein Ali Mwinyi – Chama Cha Mapinduzi (CCM),Othman Masoud Othman – ACT-Wazalendo ,Juma Ali Khatib – ADA-TADEA, Hamad Ibrahim Muhamed – UPDP, Ameir Hassan Ameir – Chama cha MAKINI ,Said Soud – AAFP, Lela Rajab Khamis – NCCR-Mageuzi ,Hasaan Juma Salum – TLP, Khamis Faki Mgau – NRA, Hamad Rashid – ADCm na Mfaume Khamis Hassan – NLD
Aidha Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar ZEC inawahimiza wagombea wote kuendesha kampeni zao kwa kuzingatia sheria, maadili ya uchaguzi, na kudumisha amani katika kipindi chote cha kampeni hadi siku ya uchaguzi.
Wagombea waliokabidhiwa vyeti na vifaa vya kampeni wameipongeza Tume kwa kuweka mazingira ya ushindani wa haki na usawa, jambo linaloimarisha demokrasia na amani katika visiwa vya Zanzibar.