Zenj FM
Zenj FM
3 September 2025, 1:49 pm

Mgombea wa uwakilishi jimbo la Tunguu, kupitia Chama Cha Mapinduzi Simai Mohammed Said akikabidhiwa fomu ya uteuzi wa uwakilishi jimbo la Tunguu na Msimamizi wa Uchaguzi wilaya ya Kati Bakari Burhan Suleiman.Na Mary Julius.
Mgombea wa uwakilishi jimbo la Tunguu, kupitia Chama Cha Mapinduzi Simai Mohammed Said, ameahidi kufanya Kampeni za kistaarabu kama ilivyoagizwa na viongozi wakuu wa chama chake.
Simai ameyasema hayo leo mara baada ya kuchukua fomu katika ofisi za Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja.
Simai ambaye amehamasika kuwania nafasi hiyo tena, amekishukuru Chama Cha Mapinduzi kwa kumteua na kumpitisha kama mgombea rasmi wa jimbo la Tunguu.
Aidha ameahidi,kupita nyumba kwa nyumba ili kuwafikia wananchi na kuwafikishia sera na mikakati ya chama hicho kwa lengo la kuleta maendeleo jimboni humo.
Simai Mohammed Said.