Zenj FM
Zenj FM
27 August 2025, 4:17 pm

Na Is-haka Mohammed.
Wananchi wa jimbo la Micheweni Wilaya ya Micheweni Pemba wameombwa kukiunga mkono chama cha CHAUMA na Wagombea wake ambao kitawasimamisha kupitia nafasi mbali mbali za uongozi katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.
Ombi hilo limetolewa na Makamo Mwenyekiti wa CHAUMMA Zanzibar Issa Abassa Hussein mara baada ya matembelezi maalum ya kumkaribisha katika chama hicho, Haji Khatib Kai ambaye amehamia chama hicho akitokea ACT Wazalendo na kuchukua fomu ya kuwania ubunge wa jimbo la Micheweni.
Amesema chama hicho kimejipanga kuingia katika uchaguzi na kupata ushindi mkubwa kwani kwa sasa ndiyo chama kinachoungwa mkono na wananchi katika maeneo mbali mbali nchini.
Akizungumza na Waandishi wa Habari huko Micheweni mwanachama mpya wa CHAUMA Haji Khatib Kai ambaye amesema kukihama chama chake cha zamani kumetokana na kutoridhika na michakato ya kuwapata wagombea ikiwemo ubunge wa jimbo hilo.
Nao baadhi ya wafuasi wanaomuunga mkono mbunge huyo wa zamani wa Micheweni akiwahudumu kwa mihula miwili wamesema kutokana na kutoridhishwa na michakato ya uteuzi wagombea ameamua kumuunga mkono mgombea huyo kwani ndiye waliyemchaguwa kuwawakilisha chama cha kwenye uchaguzi wa mwaka huu.
Jumla ya wananchama 100 waliokuwa chama cha ACT Wazalendo katika jimbo la Micheweni wamepatiwa kadi za uanachama wa chama cha CHAUMA.