Zenj FM
Zenj FM
20 August 2025, 4:16 pm

akamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman, akibonyeza kitufe kuashiria kuzinduliwa kwa mradi wa CADIR,katika ukumbi wa hotel ya Madinat al Bahr Mbweni Zanzibar.Mradi wa CADIR ni wa miaka mitano, kuanzia mwaka 2025 hadi 2029, na unafadhiliwa na Umoja wa Watu Wenye Ulemavu wa Norway (NAD), ukiwa na thamani ya Shilingi Bilioni 20 za Kitanzania.
Mradi huu utatekelezwa katika mikoa mbalimbali ya Tanzania Bara na Zanzibar, ukilenga katika maeneo ya elimu jumuishi, uwezeshaji kiuchumi, afya, marekebisho, pamoja na uhamasishaji na utetezi wa haki za watu wenye ulemavu.
Na Mary Julius.Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman, amesema licha ya juhudi za serikali katika kuboresha ustawi wa watu wenye ulemavu nchini, bado kundi hilo linahitaji msaada mkubwa na wakina.
Akizungumza katika uzinduzi wa Mradi wa CADIR, uliofanyika katika ukumbi wa hotel ya Madinat al Bahr Mbweni – Zanzibar, Othman amesema mradi huo utakuwa chachu ya maendeleo kwa watu wenye ulemavu, kwa kuongeza upatikanaji wa haki, fursa na ushirikishwaji katika nyanja mbalimbali za maisha.
Amesema ofisi yake itatoa mashirikiano ya kutosha kuhakikisha mafanikio ya mradi huo, huku akisisitiza kuwa haki za watu wenye ulemavu zinapaswa kulindwa ili kuepuka kuongezeka kwa idadi ya watu wanaopata ulemavu kwa sababu zinazoweza kuzuilika.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman.Kwa upande wake Mwenyekiti wa Shirikisho la Jumuiya za Watu Wenye Ulemavu Zanzibar SHIJUWAZA, Mwandawa Khamis Mohammed, amesema mafanikio ya mradi huo yatategemea ushirikiano wa wadau, huku akiwahimiza watu wenye ulemavu kuchangamkia fursa zitakazopatikana kupitia mradi huo.
Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya Watu Wenye Ulemavu wa Norway (NAD), Abdalla Amour,amesema mradi unatarajia,kuongezeka kwa skuli na vituo vya afya vinavyokidhi vigezo vya ujumuishwaji; ongezeko la ushiriki wa watu wenye ulemavu katika ajira na ujasiriamali; mifumo thabiti ya ushiriki wa wananchi na uwajibikaji wa watoa huduma.
Mkurugenzi Mkazi wa Taasisi ya Watu Wenye Ulemavu wa Norway (NAD), Abdalla Amour.Nae mkuu wa Wilaya ya Magharibi B, Amour H. Mmanga, ametoa wito kwa taasisi zinazohusika na watu wenye ulemavu kuongeza nguvu ili mikopo ya maendeleo inayotolewa na halmashauri iwafikie walengwa.
Aidha, amemuomba Makamu wa Rais kutoa muongozo kuhusu watu wanaowatumia wenye ulemavu kwa shughuli za kuombaomba mjini.